Samuel Sitta (kulia) akipokea fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa kudumu wa Bunge maalumu la Katiba mpya baada ya kutangazwa rasmi kwa wagombea wa nafasi hiyo kuruhusiwa kuchukua fomu wakati wa semina maalum ya kujadili kanuni iliyofungwa na Mwenyekiti wa muda Ameir Pandu Kificho leo asubuhi. Wagombe wote waliochukua fomu hizo wanatarajia kurudisha fomu baada kujaza na kesho majira ya jionu unatarajia kufanyika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa kudumu wa Bunge hilo. Kulia ni ofisa wa bunge Lydia Mwaipyana (katikati) ni Hamisi Kigwangala.
Mbali na Sitta wengine waliochukua fomu ni Theresia Huvisa, John Lifa Chipaka na Hashim Rungwe.
Mbali na Sitta wengine waliochukua fomu ni Theresia Huvisa, John Lifa Chipaka na Hashim Rungwe.
Sitta (katikati) akionesha fomu baada ya kukabidhiwa, (kushoto) ni Hamisi Kigwangala (kulia) ni Paul Makonda.
Sitta, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania Uenyekiti wa Bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Kamati ya
Uundaji wa Kanuni zitazotumika katika bunge Maalum la Katiba Prof. Costa Ricky
Mahalu akisoma azimio la kutunga na kupitisha kanuni za bunge Maalum.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba akiiunga Mkono Azimia la Kutunga na
Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
Mjumbe akiwaomba wajumbe wa bunge maalum la katiba kuunga mkono na Kupitisha Azimio la
Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba ili kuwa na umoja na
kutekeleza jukumu hili la kitaifa leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba na Naibu Waziri Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Mhagama akiunga Mkono Azimia la Kutunga na
Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba James Mbatia akiunga Mkono
Azimia la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba na kuwataka
wajumbe wengine kufanya hivyo ili kuanza kikao cha bunge maalum la katiba leo
Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Panya Ally Abdalah(mwenye
ushungi wa Bluu) akiiunga Mkono Azimia la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge
Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Sheikh. Mussa Kundecha
akiwataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Kuwa wamoja na Kupitisha Azimio la
Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Amon Muhagachi akiunga
mkono Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba na
kuwataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuunga mkono azimio kwa maslahi ya
Taifa.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Pandu Ameir
Kificho akiwaleza jambo wajumbe wa Bunge Hilo kabla ya kuahirishwa mpaka kesho
jioni na Kuwataka wale wanaotaka kuchukua fomu ya uenyekiti kuanza kuzichukua
leo.
Picha na
Hassan Silayo- MAELEZO
0 comments:
Post a Comment