Nafasi Ya Matangazo

February 13, 2014



Jeshi la polisi mkoani SINGIDA limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43.

Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika  kijiji cha MWAMAGEMBE  wilayania MANYONI  zikisafirishwa kwenda ITIGI mkoani SINGIDA.

Vitendo vya ujangili vimeendelea kukithiri nchini ambapo jeshi la plosi Mkoani SINGIDA limemtia mbaroni  GEORGE JAMES kwa tuhuma za kukutwa na meno ya TEMBO yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika kijiji UKIMBU ,kata ya MGANDU wilayania MANYONI akiwa katika gari aina ya TOYOTA HIACE lenye namba za usajili T797CQL akiwa amehifadhi men o hayo katika mabegi ya nguo.

Kamanda wa polisi mkoa wa SINGIDA ,GEOFREY KAMWELA amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani ITIGI.

vitendo vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo mwaka 2013 askari mmoja wa jeshi  polisi alipoteza maisha katika mapambano na majangili wilayani humo.
Posted by MROKI On Thursday, February 13, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo