Wakati CCM inatimiza miaka 37
tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana
mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi
hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa
habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye alisema sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa
rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein
Unguja Zanzibar.
Kilele cha sherehe hizi kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa
nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo
tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”
Sherehe hizi zitahitimishwa
hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa
Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi mbali mbali wa
Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip
Japhet Mangula ambaye pia ni mlezi wa
mkoa wa Mbeya akitanguliwa na Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi
saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa
Taifa wa Chama ,Rais Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye
jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa
Mbeya, baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine
ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki
wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya
televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
Wakazi wa Mbeya waombwa
kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi
na sherehe zitakazofanyika tarehe2.
Maadhimisho ya sherehe hizi
yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli za utunzaji wa mazingira kama kupanda
miti,kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.
0 comments:
Post a Comment