Rais wa kwanza Mzalendo na
Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ‘Madiba’ akiwa ameshikilia
viatu vyake ambavyo aliviacha nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania
kwa mara ya kwanza mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini.
Mandela aliahidi kuvichukua
viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania lakini katika safari hiyo ndipo
alipoishia mikoni mwa makaburu wa Afrika Kusini na kumfunga kwa miaka 27.
Viatu hivyo aina ya Buti
vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa Mandela na mjane wa Mzee Nsilo
Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia) mwaka 12/12/1995 Mandela alipotoka gerzani
na hatim,aye kuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment