Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto)
akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Mizinga Melu kusaidia
mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa
Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA). Hafla ilifanyika wakati wa
tukio la uzinduzi wa mradi huo unaodhaminiwa na NBC jijini Dar es Salaam
jana. Katikani ni Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika.
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto),
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Mizinga
Melu (katikati) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bi. Mwinda
Kiula Mfugale wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi wa tofuti ya vijanatz.com ikiwa na habari kuhusu ajira (kazitz.com), fedha (fedhatz.com) na ujasiriamali (biasharatz.com).
Hafla hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya
masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha
vijana nchini (TAYOA) unaodhaminiwa na NBC.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAYOA, Peter Masika (kushoto), Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), na Meneja Mkuu wa
Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe wakibadilishana mawazo katika hafla
hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAYOA, Peter Masika (kushoto), Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), na Meneja Mkuu wa
Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe wakibadilishana mawazo katika hafla
hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu akizungumza na vijana na wageni wengine
kuhusu huduma za kibenki na kuhusu mikakati ya benki kusaidia suala la
ajira na ujasiriamali kwa vijana katika hafla hiyo.
Wasanii
wakitoa burudani kusindikiza uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya masuala ya
ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini
(TAYOA) unaodhaminiwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es
Salaam
0 comments:
Post a Comment