Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2013

Mkuu wa Mawasiliano wa Katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Othieno Richard Owora akitoa mada kwenye mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari kutoka nchi za EAC yanayofanyika katika hoteli ya Imperial,Kampala Uganda .
Waandishi wakifatilia mafunzo hayo ambayo yamekua na umuhimu mkubwa wa kujenga uelewa wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mmoja wa washiriki kutoka Rwanda,Bruno Birakwate akifatilia kwa makini.
Waandishi wa habari kutoka katika nchi tano ambazo ni wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)wanapata mafunzo yaliyoandaliwa na EAC kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Ujerumani(GIZ) kuwajengea ulewa mpana wa masuala mbalimbali yanayohusu jumuiya hiyo yanayofanyika jijini Kampala nchini Uganda.
Mafunzo yamefunguliwa na Mkuu wa mawasiliano wa EAC,Othieno Richard Owora kwa kuwataka waandishi wa habari kutoa elimu zaidi kwa wananchi manufaa yanayopatikana kwenye mtengamano huo.
"Manufaa ya Jumuiya ni mengi na makubwa ukilinganisha na changamoto,ukitembelea kwenye mipaka yetu utaona wananchi kutoka sehemu moja wakienda nchi nyingine kufanya biashara hali inayodhihirisha kupiga hatua mtangamano."alisema
Mafunzo hayo ni mwendelezo wa mkakati wa EAC na GIZ kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kanda hii hatua mbalimbali za mtangamano ikiwemo Ushuru wa Forodha,Soko la Pamoja,Sarafu Moja na Shirikisho la kisiasa.
Owora ametupilia mbali kuwepo uwezekano wa kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)kwamba hoja tofauti miongoni mwa nchi wanachama zinaonesha kuelekea kwenye Jumuiya imara.Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Kenya,Rwanda,Uganda,Kenya na Burundi.
Posted by MROKI On Monday, November 25, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo