Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari
kutangaza udhamini wa Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania, (kushoto) ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Kushilla Thomas.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Kushilla Thomas (kushoto), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
kutangaza udhamini wa Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania, kulia ni Meneja wa Castle
Lager, Kabula Nshimo.
*******
Baada ya kutangazwa kwa udhamini wa miaka mitatu wa bia ya Castle Lager kwa moja ya FC Barcelona, moja ya klabu maarufu zaidi duniani, leo hii udhamini huo unazinduliwa rasmi hapa Tanzania. huu unafanyika.
Baada ya kutangazwa kwa udhamini wa miaka mitatu wa bia ya Castle Lager kwa moja ya FC Barcelona, moja ya klabu maarufu zaidi duniani, leo hii udhamini huo unazinduliwa rasmi hapa Tanzania. huu unafanyika.
Udhamini huu
unaifanya Castle Lager kuwa Bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika hususani
hapa Tanzania na nchi nyingine 10 barani Afrika ambapo Castle Lager itakuwa
kinywaji rasmi pia kwenye shughuli zote za klabu ya FC Barcelona katika nchi
hizi.
“Udhamini
utaleta manufaa mengi kwa wanywaji wa Castle Lager na mashabiki wa FC Barcelona
nchini Tanzania kupitia promosheni mbalimbali na hii itaongeza umaarufu wa timu
hii hapa Tanzania na barani Afrika kwa ujumla,” alisema Kushilla Thomas,
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania.
Hii ni mara ya kwanza kwa FC Barcelona kusaini mkataba
wa udhamini na kampuni ya Kiafrika jambo ambalo litawafungulia milango
mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania na nchi nyingine barani kuweza kupata
bidhaa, matukio ya kukumbukwa na nafasi za kushinda safari safari ya kwenda
Barcelona Hispania kuitembelea klabu.
“Tumefurahi kusaini mkataba na Castle
Lager, chapa inayofahamika dunia nzima. Tunafanana mila na desturi na Castle
Lager na sote tuna historia ya miaka zaidi ya 100. Pia kama tulivyo sisi
Barcelona, bia ya Castle Lager ina mapenzi makubwa kwaa mpira wa miguu pamoja
na mashabiki barani Afrika,” alisema Javier Faus, Makamu wa Rais wa Barcelona
anayeshughulikia Uchumi.
Castle Lager imekuwa ikijihusisha na na
mpira wa miguu barani Afrika kwa muda wa miaka 85 ambapo hivi sasa inadhamini
ligi za soka katika nchi za Zimbabwe, Swaziland na Lesotho. Pia Castle Lager ni
mdhamini wa mashindano ya COSAFA yanayofanyika Kusini mwa Afrika na CECAFA
yanayofanyika Afrika Mashariki.
Kutokana
na mpira wa Ulaya kupata umaarufu mkubwa na mashabiki barani Afrika, Castle
Lager kwa miaka mingi imekuwa mdhamini wa matangazo ya mashindano mbalimbali ya
mpira na kuwapatia mashabiki nafasi ya kuangalia mechi za Klabu bingwa Ulaya,
ligi kuu ya Uingerereza na ligi kuu ya Hispania kupitia luninga.
Watumiaji
wa CASTLE Lager pamoja na mashabiki wa FC Barcelona hapa Tanzania sasa
watarajie mambo makubwa kwani udhamini huu utawaletea mambo mengi ya kusisimua.
MASWALI
NA MAJIBU KWA MKURUGENZI WA MASOKO WA TBL, BI. KUSHILLA THOMAS
1.
Je Ushirikiano huu unahusu nini?
Ushirikiano huu unaifanya, Castle Lager kuwa Bia
rasmi Ya Afrika inayodhamini FC Barcelona.
Castle ni bia bingwa ya Afrika
ambayo inajitahidi kusimamia na kuendeleza ukamilifu/ubora wake wakati FC
Barcelona ni timu bingwa ambayo daima inalenga kufikia mafanikio zaidi. Huu ni
ushirikiano imara na ni matokeo ya mapenzi yetu kwenye soka
2. Unajisikiaje kuhusiana na ushirikiano huu?
Nina msisimko mkubwa kuhusiana na ushirikiano huu
na FC Barcelona na Nina furaha kusema kwamba ushirikiano huu utaimarisha
uhusiano kati ya Castle Lager na wateja wake wa Afrika ambao ni mashabiki
wazuri wa timu hii ambayo inaangaliwa na kufuatiliwa na wapenzi wa soka duniani
kote.
3. Castle itafaidika vipi na ushirikiano huu?
Kupitia ushirikiano huu, Castle Lager itakuwa ni
bia pekee Afrika yenye haki za kipekee kutumia Nembo ya FC Barcelona,
rangi, na picha za wachezaji katika mawasiliano ya bidhaa ya Castle kama vile
matangazo ya aina zote nk. Tunaamini kwamba ushirikiano huu Utajenga uhusiano kati
ya FC Barcelona na watumiaji wa bia ya Castle Lager. Aidha kutakuwa na
shughuli mbalimbali zinazohusu kuendeleza mpira Tanzania zikiendelea na
maeneo mengine ya Afrika inakopatikana bia ya Castle.
Bia ya Castle inatambuliwa kama mdhamini Mkuu wa mpira
wa miguu na matukio mengine mengi ya michezo Afrika na kimataifa. Ushirikiano
huu kati ya Barca / Castle ni kilele cha mafanikio ya udhamini wa
michezo.
4. Ina maana gani kwa
mashabiki wa soka na watumiaji/wateja wa CASTLE katika
Nchi yako?
Tunataka kuhakikisha kwamba tunaimarisha undugu huu
katika soka la Tanzania na hasa mashabiki wa FC Barcelona ambao ni sehemu ya
ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo zaidi yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi
wa kitaifa jijini Dar es Salaam tarehe 17 Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania
watashiriki katika mfululizo wa shughuli za soka za kikanda / kanda ambazo ni
za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za kijamii, kuwazawadia mashabiki wetu
waaminifu wa Castle/Barca. Kupitia ushirikiano huu Castle Lager itahakikisha
kila shabiki anafurahia wakati kamili
5. Je Ushirikiano huo
utakuwa na manufaa chanya kwenye jamii Nchini kwako?.
Hakika, Mashabiki wa Barcelona Tanzania na jamii
zao kuna mengi ya kusuburia, Castle Lager ina mipango mikubwa ya kuifikia jamii
kwa maendeleo kwenye mikoa zaidi ya nane nchini.
Tunataka kuhakikisha kwamba tunaimarisha undugu huu
katika soka la Tanzania na hasa mashabiki
wa FC Barcelona ambao ni sehemu ya ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo zaidi
yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini Dar es Salaam tarehe 17
Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki katika mfululizo wa shughuli
za soka za kikanda / kanda ambazo ni za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli
za kijamii kuwazawadia mashabiki wetu waaminifu wa Castle/Barca. Kupitia
ushirikiano huu Castle Lager itahakikisha kila shabiki anafurahia.
0 comments:
Post a Comment