Nafasi Ya Matangazo

July 18, 2013

Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi. 
 **********
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umezindua huduma mpya za kidijitali zinazowawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi kupata huduma za RITA kwa kutumia simu zao na hivyo kupunguza gharama.

RITA, ambayo ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria, imezindua huduma hizo jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Julai 18, 2013) ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki.

Huduma za Simu Kupitia ‘sms’
Kwa wateja wa RITA wenye simu za mkononi na ambao wangependa kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma zetu bila kufika katika ofisi zetu, watapaswa kutoa namba zao za simu za mkononi , namba hizo zitaingizwa katika Kanzi ya RITA (RITA Database) na hivyo RITA kuweza kuwasiliana na wateja kwa njia ya simu kila panapohitajika.

Baada ya namba hio kuingizwa katika Kanzi (Database), RITA itakuwa inawasiliana na mhusika moja kwa moja kwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms) popote alipo kwa kumpa taarifa za huduma zetu na kujibu maswali yake bila ya yeye kufika katika ofisi za RITA.


Kupata Taarifa fupi ya ‘sms’ kuhusu Usajili wa Vizazi na Vifo
Kuanzia sasa, mteja wa RITA mwenye simu ya mkononi na anayetaka kujua kwa ufupi namna ya kusajii matukio kama vizazi na vifo, anaweza kutuma neno RITA kwenda namba 15584 (gharama ya sms Tsh 200 tu) na atapokea mwongozo utakaomwezesha kujua utaratibu wa kusajili kizazi au kifo kilichotokea hospitali na kwengine.

Kupata Taarifa fupi kuhusu ombi la cheti cha kuzaliwa
Aidha, RITA imeanzisha huduma ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (sms) ili kuwawezesha wateja kupata ‘sms’ pindi maombi yao waliyowasilisha RITA kuhusu huduma mbalimbali yanapokua yamekamilika. Maombi haya ni kama yale ya vyeti vya kuzaliwa baada ya kujaza fomu na kufanya malipo stahiki.

Anachotakiwa kufanya mteja wa RITA mwenye simu ya mkononi ni kutuma neno CHETI kwenda namba 15584 na atapokea ujumbe mfupi (sms) utakaomjulisha kama cheti chake kiko tayari ama bado. Wateja wanaopaswa kutuma ujumbe huu ni wale ambao wamekamilisha taratibu zote ikiwemo kujaza fomu na kufanya malipo stahiki.

Aidha, kwa wale wateja ambao hawatatuma ujumbe na namba zao za simu zipo katika Kanzi (Database) ya RITA, watatumiwa ujumbe mfupi kuwa vyeti vyao vipo tayari ili wavichukue mara baada ya vyeti hivyo kuchapwa.

Huduma za RITA kupitia ‘Tovuti na Mitandao ya Kijamii”
Tunataka kuwa karibu zaidi na kushirikiana na umma, kwa kutumia tovuti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi kama njia ya kuwasiliana na kusambaza taarifa muhimu kwa wananchi.

Kutokana na ongezeko la watumiaji wa intaneti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi, RITA iko tayari kwenda sambamba na mabadiliko hayo na kutoa jukwaa la mawasiliano baina yetu na wananchi. Tovuti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi ni njia rahisi ya kuweza kuwafikia wananchi wetu walioko ndani na nje ya Nchi kwa kutoa taarifa muhimu na kuwajibu maswali mbalimbali kuhusu huduma zetu. Kupata huduma hizi wa watumiaji wa intaneti ni rahisi:

Huduma hizi zina lengo la kupunguza gharama na usumbufu
Ni matumaini ya RITA kuwa matumizi ya huduma hizi yatasogeza huduma zetu karibu zaidi na wananchi wote, walio ndani na nje ya nchi. Aidha, huduma hizi zitapunguza usumbufu na gharama za kusafiri hadi katika ofisi za RITA kwa ajili ya kupata taarifa au majibu ya maswali . Pia, huduma hizi zitawapa fursa wananchi na wateja wa RITA kuwasilisha maoni au malalamiko yao kwa urahisi kupitia mitandao ya kidijitali.
Posted by MROKI On Thursday, July 18, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo