Ofisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp Limited, Hussein Mbululo, akizungumza
na waandishi wa Habari kuhusiana na huduma mbalimbali za kibenki zinazopatikana
katika katika Banda la Benki hiyo lililopo katika viwanja vya Maonesho ya
Kimataifa ya Biashara ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius
Nyerere barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo (kulia) akizungumza na Wafanyakazi wa Benki hiyo waliopo Viwanja vya Maonesho sabasaba, Ofisa Masoko, Adebert Archerd na Katikati ni Ofisa Uendeshaji wa shughuli za Kibeki wa Twiga Bancorp, Upendo Tendewa
Wakazi wa Dar es Salaam wakiingia katika Banda la Karume lililopo jirani nja Banda la Twiga Bancorp.
Mteja akipata huduma ya kuchukua Fedha katika mashine ya kutolea fedha ya Umoja Switch, hivyo wateja hawana haja ya kutembea na Fedha katika maonesho hayo. Wateja wakipata huduma na ushauri ndani ya banda hilo. Ofisa Uendeshaji wa shughuli za Kibeki wa Twiga Bancorp, Upendo Tendewa, akihudumia wateja walio fika katika banda la Twiga Bancorp kufanya shughuli za Kibenki.

********
BENKI
YA Twiga Bancorp kuanzia mwezi oktoba mwaka huu inaanza kutumia
mawakala nchini ili kutoa huduma za kibenki kwa nia ya kupanua
huduma zao kwa wananchi na kuongeza idadi ya watumiaji huduma za kibenki.
Kutokana
na utumiaji wa mawakala kuanzia juzi benki hiyo imebadili taratibu zake
za kibenki na wanaendelea na kupanga taratibu kufikia leo hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji mkuu wa benki hiyo,Hussein Mbululo alisema hayo jana katika badna la
maonesho lililopo viwanja vya sabasaba katika maonesho ya 37 ya biashara ya
kimataifa yanayoendelea .
Alisema
katika kuanzisha utaratibu huo wa kuwa na mawakala hao watawapatia vifaa
katika kufanya huduma hizo za utaratibu wa kibenki huku wakihakikisha wakala
ana duka lililopo maeneo yenye usalama.
“awali
tulikuwa na mkakati wa kufungua kila mwaka tawi moja katika mikoa tofauti
pamoja na kutumia vicoba lakini sasa tunapanua wigo kwa kutumia mawakala
mbalimbali ifikapo mwezi huo”Alisema
Alisisitiza
kuwa mwaka huu wamefungua tawi mkoani Dodoma huku wakitoa huduma ya kila wiki
kwa vicoba katika wilaya ya Bunda
AKizungumzia
maonesho hayo alisema wao wanashiriki kwa kuelezea huduma zao pamoja na kutoa
huduma zote za kibenki huku wanaotumia huduma ya ATM za umoja wakipata huduma
katika ATM zao.
Ili
kukabiliana na wizi wa mitandao ,Mkurugenzi huyo alisema wamegundua kuwa kadi
zao zilikuwa hazina ubora wa kutosha hivyo kutoa mwanya wa kufanyika kwa wizi
hivyo wameamua kubadilisha kadi na kutengeneza zenye ubora zaidi.
Alisema
benki hiyo iliishaibiwa kwa wizi wa mitandao zaidi ya sh.milioni 30 na
kufanikiwa baadhi ya wezi hao kuwapata na sasa wamedhibiti mianya yote ya wizi.
“baada
ya kuibiwa tulibaini kuwa kadi zetu zilikuwa na ubora wa chini hivyo
tumezibadili na kuhakikisha muda wote benki zatu zinakuwa na ulinzi wa kutosha
“Alisema .
0 comments:
Post a Comment