Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar ambapo alitembelea mabanda mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed (kushoto) akimkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwenye Banda la HSC kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiangalia baadhi ya bidhaa zenye ubora zinazouzwa na Kampuni ya HSC katika maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia kifaa cha kusafishia mazulia jinsi kinavyofanya kazi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed na baadhi ya wafanyakazi wa HSC katika Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Sabasaba.
Umati wa wakazi wa jijini Dar es Salaam ukiwa umefurika kwenye Banda la Home Shopping Centre kujipatia mahitaji mbalimbali ya nyumbani.
Mtsahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya jinsi Mfuko wa Fursa sawa kwa wote unavyopambana na kutokomeza Ugonjwa wa Saratani ya Matiti kwa wakina mama nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal walipokutana kwenye Banda la Mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa akiagana na Mstahiki Meya Jerry Silaa mara baada ya kutembelea Banda la (EOTF) linalotoa fursa kwa wajasiriamali nchini Tanzania kuonyesha bidhaa zao katika maonyesho hayo kila mwaka.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipata maelezo jinsi ya kutumia Kizimamoto Fanisi cha kurusha (Fire Extinguisher) ambacho ni rahisi kutumia na hakihitaji matengenezo na hudumu kwa miaka mitano pia Kifaa hicho ni rafiki wa mazingira na mvumbuzi bora kwa uokoaji wa dharura wakati alipotembelea Banda la GreenBat Fire Solutions katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea.
Mstahiki Meya Jerry Silaa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa GreenBat Fire Solutions.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika banda la Arusha International Conference Centre (AICC) wanaoshughulika kutoa huduma za kumbi za Kimataifa za mikutano na Utalii jijini Arusha.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia jinsi mtoto Range Jackson ( wa pili kushoto) mwenye ulemavu wa Ubongo akionyesha ramani ya Tanzania na Sehemu ya mipaka yake iliyotumika kumfundishia kujua kusoma na kuandika na ufundi stadi kupitia kituo cha VETA. Kulia ni Mkufunzi wa kuchomea (Welding Instructor) na Mwalimu wa watu wenye mahitaji maalum Bw. Kintu Kilanga na Wa tatu kulia ni Baba mzazi wa kijana huyo Bw.Jackson Range.(Picha na Zainul Mzige).
0 comments:
Post a Comment