MBUNGE WA Kigoma Kaskazini, Ndugu Zitto Z. Kabwe amealikwa kuhudhuria tamasha la tisa la Aspen la mwaka
huu huko Marekani. Tamasha hilo linawaleta pamoja watu mashuhuri kutoka nyanja
mbalimbali duniani.
Lengo kubwa la tamasha ni kuwawezesha washiriki kubadilishana mawazo kuhusiana
na masuala mbalimbali ambayo wana uzoefu nayo.
Ushiriki katika tamasha hilo utamwezesha Zitto kukutana na kubadilishana
mawazo na magwiji wa masuaka mbalimbali duniani.
Ratiba iliyotolewa na waandaaji inaonyesha kuwa tamasha hilo litakaloendeshwa
kwa muda wa wiki moja kuanzia Juni 26, limegawanyika katika sehemu mbili.
Kama ilivyo kwa miaka iliyopita, tamasha hilo litahusisha majadiliano ya
pamoja, ya vikundi pamoja na ya mtu mmoja mmoja.
Pia washiriki watakuwa na fursa ya kukutana na wabunifu na wataalamu wa nyanja
mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.
Mijadala itahusu mambo ya kijamii, siasa, mahusiano ya kimataifa, watoto
na vijana pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili
dunia hivi sasa.
Vile vile kutakuwa na maonyesho ya vitabu pamoja na mikutano na waandishi
wa habari maarufu kutoka Marekani. Washiriki pia watapata fursa ya kujifunza
kupitia filamu na michezo ya kuigiza.
“Nimefurahi kupata mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu kwangu
mimi hii ni nafasi adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa masuala mbalimbali,
pia ni fursa kubwa ya kueleza maoni yangu kwa waalikwa mbali mbali. Nina
uhakika kuwa watu nitakaokutana na kubadilishana nao mawazo na uzoefu
watasaidia kupanua uelewa wangu wa masuala kadhaa”, alisema Zitto alipotakiwa
kufafanua umuhimu wa tamasha hilo kwa vijana.
Baadhi ya watu maarufu watakaotoa mada katika tamasha hilo ni pamoja na Majaji
washiriki wa Mahakama Kuu ya Marekani Stephen Breyer na Elena Kagan, Mwakilishi
Eric Cantor, Rais wa Kituo cha Brady Dan Gross, Rais wa Chama cha Wamiliki wa
Bunduki Marekani David Keene, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice;
Rais wa Taasisi ya Taasisi ya Kulinda Rasilimali, Frances Beinecke;
Mkurugenzi mwenza wa Boies, Schiller & Flexner LLP David Boies,
Waziri wa kazi wa zamani Elaine Chao, Waziri wa Usafirishaji Ray LaHood, Meya
wa New Orleans Mitch Landrieu, Waziri wa Fedha wa zamani Hank Paulson, Gavana
wa zamani wa Minnesota Tim Pawlenty, Mshauri wa Chama cha RepublicanKarl Rove na Rais wa Shirikisho la Walimu Marekani Randi Weingarten.
http://www.aspenideas.org/content/2013-scholars
0 comments:
Post a Comment