Redd's Miss Tanzania, Brigitte Alfred (katikati) akiwa sambamba na Mshindi wa Pili wa Taji hilo Eugenia Fabian (kushoto) na Edna Sylvester wakati warembo hao walipo twaa nafasi tatu za juu za Redd's Miss Tanzania 2012. Leo warembo hao wote wanavua mataji yao ya vitongoji.
****** ******
Na Father Kidevu Blog.
Wakati shindano la Redd's Miss Tanzania 2013
likizidi kushika kasi kwa vitongi vingi na mikoa kumalizia mashindano yao na
kubaki Ngazi ya Kanda na Taifa leo kivumbi kina waka kwa warembo kadhaa
kuchuana vikali kuwavua mataji washindi wa tatu bora ya Miss tanzania 2012.
Hapo Sinza warembo 12 watapanda jukwaani kuwania
taji la kitongoji hicho linaloshikiliwa na Redd's Miss Tanzania 2012 Brigite
Alfred analishikilia.
Huko Mara napo kutakuwa na mchuano mkali kwa
warembo 12 nao kupanda jukwaani kuwania taji linaloshikiliwa na Redd's Miss
Tanzania namba 2, Eugen Fabian.
Ndani ya jiji la Dar es Salaam tena kutakuwa na
patashika ya sketi kuchanika pale katika Kitongoji cha Kigamboni City ambapo
warembo wengine 12 watawania taji la kitongoji hicho linaloshikiliwa na Redd's
Miss tanzania namba tatu Edna Sylvesta.
0 comments:
Post a Comment