Wakili Froldius Mugisha Mutungi (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakili Emmanuel Tamila Makene (wapilikushoto) pamoja na Mkewe mama Mutungi na kijana kutoka Ofisi ya Kings Low Chember, Daudi.
*********
Ama kweli penye nia njia
hupatikana….
Msemo huu wa wahenga
umekamilika tarehe 21 Juni 2013 ambapo Ndugu Froldius Mugisha Mutungi
ameapishwa kuwa wakili wa kujitegea.
Muuguzi huyu anamshukuru sana Mwenyezi
Mungu kwa kumpa afya ya mwili, roho na akili pia. Na anawashukuru sana familia
yake hasa mke wake ,wafanyakazi wenzake, ndugu jamaa na marafiki ambao wamemsaidia
kwa njia moja au nyingine hata kupatikana mafanikio haya.
“Hakika ilikuwa safari ndefu
iliyojaa milima na mabonde mpaka kufikia hapa nilipo. Inahitaji kuwa na malengo
,ujasiri na uthubutu, kujituma na kuwa na dhamira ya kweli ili kuyafikia
malengo. Ni safari ambayo inahitaji kujitoa sadaka kwa mambo mengi kuanzia
familia,ndugu jamaa, marafiki shughuli za kijamii na hata kazi. Wakati mwingine
inahitaji kuweka rehani baadhi ya mambo muhimu ili kusonga mbele.
Katika safari kama hii
inahitaji uwe na msimamo wa kusimamia maamuzi yako. Nilipoanza chuo mwaka 2006
pale Chuo Kikuu Huria cha Tanzania baadhi ya watu tena wengine watu wangu wa
karibu walinikatisha tama lakini wapo walionitia moyo.
Namshukuru sana mke wangu alinielewa pamoja na
kwamba nilimwachia mzigo mkubwa wa kuendesha familia wakati niko shule hasa
wakati nasoma shule ya sheria. Kazinin nako mambo hayakuwa rahisi lakini kwa
kuwa nia nilikuwa nayo, sababu nilikuwa nazo na uwezo pia nikuwa nao nilibakiza
kazi moja tu, kusoma na kufaulu.
Tangu nikiwa mdogo sikupenda
kuona mtu anadhulumiwa au kunyanyaswa, nilipenda sana haki.Lakini baba yangu
Mzee John Mutungi aliwahi kuniambia kuwa “haki haipatikani kirahisi na ina
gharama, tena gharama kubwa kwelikweli…” Sikumelewa wakati huo alichomaanisha.
Nilipofika kazini kama Afisa Muuguzi Msaidizi
nilikuta mambo ni tofauti na nilivyotegemea.Nilitafuta njia ya kuwatetea wanyonge
lakini kila mara nilikwaa visiki. Nilipotafakari sana, nadhani Mungu
akaniongoza nisome sheria kwani hata nilipokwenda chuo kuchukua fomu za
kujiunga sikuwa nimefikiria kusoma sheria.
Leo sasa yametimia, Mungu
amejibu maombi, “ hakika ameutazama unyonge wa mjakazi wake”. Naweza sasa
kuwasemea na kuwatetea wanyonge wasioweza kujisemea au kujitetea.
0 comments:
Post a Comment