WAKATI bado wasanii na wapenzi
wa burudani nchini Tanzania wapo katika majonzi kufutia kifo cha Msanii Albert
Mangweha, leo tasnia ya Maigizo na Filamu nchini wamefikwa na janga lingine la
kufiwa na Msanii Jaji Khamisi au Kash.
Muigizaji huyo wa filamu na
muigizaji Kashi amefariki dunia mchana huu katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Kashi amewahi kutamba na mchezo mbalimbali
ya kuigiza katika vituo vya televisheni vya Stars TV akiwa na kundi la Getwell
Generation lililokuwa likicheza mchezo wa Hapa ni Bongo na baade kuhamia Kaole
na kuonekana ITV akiigiza mchezo wa tamu Chungu na mwisho kuingia katika uchezaji filamu za bongo maarufu Bongo
Movie.
Akizungumza kwa majonzi msanii
mwenzake ambaye waliigiza wote katika kundi la Getwell Generation na baadae
kuhamia nae Kaole, Halima Yahaya 'Davina' amesema ni kweli Kashi amefariki.
Davina amesema yeye alipta
taarifa za kuumwa kwa Kash jana usiku na leo alikuwa akijipanga kwenda
kumsalimia Hospitali Muhimbili lakini ghafla akapokea taarifa kuwa Kashi
amefariki.
Aidha Davina amesema msiba upo
Kinondoni jirani na Bar ya Katumba, jijini Dar es Salaam ambapo mipango ya mazishi
inafanyika.
Akimwelezea marehemu msanii Umy
Wenselaus 'Dokii' aliyekuwa kiongozi wa kundi la Getwell na mwalimu wa Maigizo
wa kwanza wa msanii huyo amesema kuwa marehemu alikuwa muigizaji mwepesi na
aliye na kipaji.
"Ni pigo katika tasnia ya
Maigizo maana Marehemu alikuwa na kipaji na mwepesi sana kushika vitu
anavyopewa kuvifanyia kazi na hubadilika kulingana na hali ya
mchezo,"alisem,a Dokii.
Katika siku za hivi karibuni
tasnia ya maigizo imekumbwa na misiba ya kuondokewa na wasanii wake kama Steven
Kanumba, Mzee Kipara, Sharo Milionea, Mlopelo na Haji Maganga.
0 comments:
Post a Comment