Ikiwa ni takribani siku kumi tu tangu mauti yamfike Msanii Albert Mangweha a.k.a Mimi tayari CD na VCD za kazi zake zimeanza kuuzwa mitaani kama njugu hasa katika maeneo mbalimbali ya mikusanyiko na mataa ya magari. Lakini swali la Father Kidevu Blog na mtanzania yeyote yule anae jali maslahi ya msanii je Familia ya Marehemu inafaidika nini na kazi hizi za mpendwa wao.
Bila shaka Baraza la Sanaa la taifa na COSOTA wanaweza toa majibu stahiki juu ya mapato hayo na endapo mtengenezaji ana kibali cha familia au Mtayarishaji wa kazi za marehemu.
0 comments:
Post a Comment