Mahmoud
Ahmad Arusha
Mkuu wa mkoa
wa Arusha Magessa Mulongo amevitaka vyama vya wafanyakazi kuwachunguza
waajiri wanao kiuka sheria za kazi kwa kuajiri kwa miezi mitatu mitatu
kwani wamekuwa wakiwaacha
wafanyakazi kama walivyowaajiri mwanzo bila ya mafao ya mwisho wa kazi.
Mulongo ametaka waajiri waaina hiyo wasiofuta sheria za kazi kuanza kufanyiwa
uchunguzi haraka.
Kauli hiyo
ameitoa kwenye kilele cha siku ya wafanyakazi kwenye viwanja vya kumbu kumbu ya
Sheikh Amri Abeid jijini hapa na kusema kuwa wapo waajiri wa aina hiyo wengi
wasiojali maslahi ya wafanyakazi na mwisho wa siku kuwaacha hawana mafao yeyote
huko ni kuwaumiza wafanyakazi.
Mulongo
alisema kuwa kumekuwapo na wahitimu ambao wenye stashahada na Diploma wamekuwa
wakiongoza kwa utendaji mzuri wa kazi wakati wenye digrii wakiwa hawana uzoefu
na moyo wakuifanyakazi na kubaki kupiga fitna na wakati wakiwa vyuoni walikuwa
wakifuatilia siasa na kuacha kufuta taaluma zilizowapeleka vyuoni humo.
“Ndugu zangu
wafanyakazi wenzangu Taaluma yeyote inahitaji muda mzuri wa kuifuatilia tangu
ukiwa chuoni hadi unaingia kazini sasa hapa upo chuoni unaacha taaluma unafuata
mambo yasio ya taaluma huku ni kutokuwa na wataalamu wa kufaa hapo ndipo fitna
zinapoanzia”alisema Mulongo.
Mulongo
alienda mbali na kuwataka wanahabari kuandika habari kufuatana na taaluma zao
na kuacha ushabiki wa kisiasa kwani taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma
yenye weledi na ina miiko na maadili hapa ndugu zangu tuelimishe jamii masuala
ya kimaendeleo badala ya kijikita kwenye masuala ya kisiasa zaidi na kuicha
nchi ikielekea kwenye lingi la vurugu.
“ipo wakati
mtajikuta mkiangukia kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma mbali mbali kwani
mtakuwa mmeacha taaluma na kuuvaa ushabiki wa kisiasa hapo mtakuwa hamuitakii
nchini yenu maendeleo bali mtakuwa mnaitakia nchi yenu mabaya”alisema mkuu wa
mkoa.
Sherehe hizo
zilienda sambamba na maandamano ya vyama vya wafanyakazi na makampuni mbali
mbali huku maonyesho ya magari yakitia for a hasa kampuni ya Megatrade
Investment watengenezaji wa Kiroba orgin na Kvant Gin na Kiwanda cha Banana
Ivestment Huku kwenye viwanda vya kutengeneza nguo Kampuni ya AtoZ ikitia for a
ikifuatiwa na kampuni ya Sunflag zote za jijini hapa.
0 comments:
Post a Comment