TAARIFA za
awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka
gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam
inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China
kufuata bidhaa za maduka yake.
Shirima (47),
ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara
aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na
Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha
taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si
msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa
Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio
inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo
baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.
Inadaiwa
kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo
aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na
gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.
Marehemu
Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa
akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.
Marehemu
ameacha Mjane na watoto 5.
Uchunguzi
wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili
zitatolewa pindi zitakapo kamilika. Timu nzima ya Father Kidevu Blog inatoa
pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo.
Rip
ReplyDeleteINASIKITISHA SANA, INAONEKANA ALIPOPANDA JUU KUPATA HEWA AKAPATWA NA KIZUNGUZUNGU NA PENGINE ALIKUWA KWENYE EDGE YA JENGO NDO AKADONDOKA, WHAT A SAD STORY. APUMZIKE KWA AMANI. AMINA
ReplyDeleteJamani!! Poleni sana ndugu wa Shirima mliopatwa na Msiba huo. Siri yake anayeijua ni Mungu tu. Mungu amlaze mahali pema peponi Amen!!
ReplyDelete