Nafasi Ya Matangazo

May 24, 2013

WAKATI jumla ya warembo 13 wamejitokeza kuwania taji la Redds Mid Sinza 2013 iliyopangwa kufanyika Juni 7, kwenye ukumbi wa Meeda Club, kampuni ya Tanzania Distillers Limited (TDL),  kinywaji cha Chilly Willy na kampuni ya  CXC Africa zimejitokeza kudhamini mashindano ya Redds Miss Sinza 2013 yaliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi w Meeda Club Juni 7.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema jana kuwa TDL imedhamini mashindano hayo kupitia kinywaji chake cha Dodoma Wine ambao pia mwaka jana walidhamini mashindano hayo.
Majuto alisema kuwa wamepata faraja kubwa mwaka huu baada ya idadi ya warembo kuongezeka sambamba na wadhamini. Wadhamini wengine ni kampuni ya TBL kupitia Redds Original, Clouds FM, Fredito Entertainment,  Sufiani Mafoto Blog na Saluti5.
Alisema kuwa warembo wameitikia wito katika mashindano hayo kwani wanataka kutwaa taji la Miss Redds Miss Tanzania ambalo Sinza ni watetezi kupitia mrembo wake Brigitte Alfred.
“Bado tunahitaji warembo zaidi ili kupamba shoo yetu ambayo ni ya mwisho kwa kanda ya Kinondoni. Pia tunawaomba wadhamini wengine kujitokeza kwani Miss Sinza 2013 ni zaidi ya promosheni na burudani,” alisema Majuto.
Mpaka sasa warembo 13 wamejitokeza katika mashindano hayo na wapo mazoezini chini ya Miss Tanzania Top Model, Mwajabu Juma.
Posted by MROKI On Friday, May 24, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo