Profesa Lipumba, akiiangalia
ukuta uliojengwa na wananchi wa Kijiji cha Kigombe mkoani Tanga, mara baada ya
kuuzindiwa, kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mzee Said. Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kigombe Mzee Said, akitoa maelezo kwa Profesa Lipumba kuhusu ujenzi wa
kingo ya Bahari ambao umejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa thamani
ya Sh milioni 108.
***** ******
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MWENYEKITI wa Chama cha
Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Mkoa wa Tanga ni moja kati ya
mikoa maarufu kwa viwanda nchini lakini hivi saa hali ya kimaendeleo katika
mkoa huo imekuwa mbaya.
Kauli hiyo ameitoa leo mjini
hapa alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu maendeleo ya uchumi kwa Mkoa wa
Tanga katika kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kwa
kushirikiana Taasisi ya Maendeleo ya demokrasi kwa vyama vya siasa ya nchini
Denmark (DIPD).
Profesa Lipumba alisema
kuwa hakuna haki bila kuwa na maendeleo yanamgusa mwananchi wa kawaida.
Alisema Mkoa wa Tanga
imefanikiwa kuwa na rasimali nyingi ikiwemo zao la Mkonge ambalo kwa sasa limekosa
msukomo hali inayochangia umaskini kwa wananchi wa mkoa huo.
"Pamoja na Tanga kuwa na
fursa nyingi za kiuchumi lakini bado kadri siku zinavyokwenda umaskini umekuwa
ukiwatesa wananchi. Viwanda vilikuwa zaidi ya 70 lakini sasa hakuna hata kimoja
kinachofanya kazi huku zao la mkonge lilikosa msukumo wa makusudi kwa wananchi
wake.
"Katika soko la dunia
inaonyesha kuwa Tanga ilikuwa ikizalisha tani 234,000 kwa mwaka lakini sasa
mkonge umeporomoka na kufikia tani 25,000 tu hali ambayo imekuwa ikiongeza umaskini
kila kukicha. Kama kungekuwa na msukumo wa makusudi wa kufufu zao hili ni wazi
Tanga ingekuwa imepaa kimaendelo kwa wananchi wake kutokana na kuwa na kila
aina ya rasilimali zikiwemo za matunda na mbogamboga," alisema Profesa
Lipumba
Profesa Lipumba, ambaye ni
mtaalamu wa masuala ya uchumi duniani, alisema ili kuweza kufikia malengo ya
mkoa huo kuweza kupambana na umaskini ni lazima serikali ikubali kwa kufanya
uwekezaji hasa katika kufungua bandari ya Tanga ambayo ni lango kuu la
kiuchumi.
Alisema Bandari ya Tanga
imekuwa haitumiki ipasavyo hali inawechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa
umaskini na hazorotesha harakati za mkoa na wananchi kwa ujumla.
"Bandari ya Tanga, zao la
mkonge pamoja na kukosekana kwa msukumo wa kuimarisha sekta ya elimu ni moja ya
masuala yanayoufanya mkoa huu kuzidi kurudi nyuma kiuchumi pamoja na wananchi
wake,” alisema Profesa Lipumba.
0 comments:
Post a Comment