Mtaalamu wa kutoa damu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mpango wa Damu Salama, Linus Kupuya akimtoa damu mmoja wa waumini wa Kanisa la Adventista Wasabato, Dolka Juma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Huduma na Matendo ya Huruma kwa Jamii Ulimwenguni. Sherehe hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni wiki.
DAR ES SALAAM, Tanzania
WAUMINI wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania
wameungana na waumini wenzao ulimwenguni kusherehekea siku ya huduma na matendo
ya huruma kwa jamii ambayo yaliadhimishwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.
“Kwa kuzingatia umuhimu wa siku hii waumini wa kanisa duniani
kote wametembelea maeneo mbali mbali kwa ajili ya kutoa misaada kwa wahitaji
ikiwa ni pamoja na kuchangia damu katika benki ya Damu salama, kutembelea hospitali,
kutoa misaada kwa wagonjwa, kutembelea vituo vya watoto yatima, kituo cha
kijiji cha watuwasiojiweza Msimbazi center, mahabusu ya watoto upanga na
magereza,” alisema.
Mchungaji Sunwa alitaja maeneo yaliyotembelewa kuwa ni Mwananyamala, Muhimbili, Amana,Temeke, Lugalo, Nevy, Parestina,
Mbwenimission, Ocean Road, Vijibweni Kigamboni, Mabagala Zakiena, Tumbi Kibaha, Dar group na vituo
vya watoto yatima Bunju,Ungindoni na mburahati.
Pia mchungaji huyo aliwataka Watanzania kuwa na moyo wa
kujitolea pale panapohitajika hasa kwa watu wasiojiweza na watoto wanaoishi
katika mazingira magumu.
0 comments:
Post a Comment