Mmoja wa waendesha kipindi cha Guinness Football Challenge Larry Asago.
Jana
usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV mashindano ya GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE™ yalituonesha ni kwanini ushirikiano ni muhimu kwa washiriki kuonyesha ujuzi wao. Francis Ngigi
and Kepha Kimani kutoka Kenya walifanikiwa kuingia hatua ya mwisho na kujipatia fedha za kimarekani dola 3,000 shukrani kwa vipaji vyao na
ushirikiano mzuri.
Francis
na Kepha wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya
Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano
haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya
zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa
kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa
ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika
televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi
kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15)
usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .
Tafadhali kunywa
kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
0 comments:
Post a Comment