Nafasi Ya Matangazo

March 28, 2013


Kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee  moja ya kikundi kitakachotumbuiza katika Matamasha ya Airtel Yatosha akiongea wakati wa uzinduzi wa Matamasha hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel morocco, Matamasha haya yatawashirikisha wasanii wengine wakiwemo Fid Q,   Juma Nature,   Ney wa Mitego  na Stamina.Kulia Meneja Mauzo Airtel  Kanda ya Pwani  Raphael Daudi



Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati akitangaza wa Airtel wa kufany Matamasha ya Airtel Yatosha katika mikoa mbalimbali ya Tanzania yenye lengo lan kutoa burudani sambamba na kuelimisha Jamii na wateja  wake kuhusu huduma za Airtel ikiwemo kuitambulisha huduma mpya ya Airtel Yatosha. Kulia Meneja Mauzo Airtel  Kanda ya Pwani  Raphael Daudi

*****       ******
Airtel Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kufanya matamasha ya Airtel Yatosha yenye lengo la kutoa burudani na kuwaelimisha jamii na wateja wake  juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel ikiwemo huduma mpya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa gharama nafuu zaidi.

Akiongea wakati wa kutambulisha matamasha hayo, meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kutoa burudani wakati wa msimu huu wa sikukuu ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma yetu ya Airtel yatosha kwa watanzania,  tunaamini kwa kupitia matamasha yatakayofanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania wateja wetu na watanzania kwa ujumla watapata burudani na kupata nafasi ya kupata elimu juu ya huduma zetu Nyingi


“Safari yetu ya burudani za Airtel yatosha itaanza katika Mkoa wa Morogoro katika siku ya  Jumapili na Jumatatu ya Tarehe 31/3 na 01/04/2013,  Kuanzia Saa Tatu kamili Asubuhi mpaka saa Kumi na Mbili Jioni, pale katika viwanja vya Sabasaba.

Tutakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Fid Q,   Juma Nature,   Ney wa Mitego  na    Tip Top Connection. Kiingilio ni BURE , tunapenda kukukualika wewe na washikaji zako wote kuhudhuria katika tamasha hili la kwanza kabisa pale morogoro na utape burudani kabambe. Njoo na Kitambulisho chako ili uunganishwe na ufurahie ofa nyingi toka Airtel” aliongeza Mmbando .

Naye kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee  alisema” kama kawaida tumejipanga kuwapa wateja wa Airtel na watanzania burudani ya Ukweli katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika matamasha haya ya Airtel Yatosha. Mbali na sisi kutoa burudani itakuwa nafasi pia kwetu kuona vipaji mbalimbali vya mashabiki wetu ambao ndio wasanii nyota wa kesho hivyo tuwapa hamasa ya kujitokeza kwa wingi ili tuweze kuburudika pamoja.

Wasanii watakaoshiriki katika Matamasha maalumu ya Airtel yatosha watatumbuiza kwa vibao vyao mahiri kama vile Fid Q na kibao chake cha Sihitaji Marafiki na  Ney wa Mitego na kibao chake cha Nasema Nao huku Tip Top Connection wakiwakilisha na kibao chao cha Nani kamwaga pombe yangu.

Airtel hivi karibuni imezindua huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha  mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.  Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99# 
Posted by MROKI On Thursday, March 28, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo