MECHI YA TAIFA STARS YAINGIZA MIL 226/-
Mechi ya mchujo ya Kombe
la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars)
na Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jana (Machi 24 mwaka huu) na Stars
kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 226,546,000.
Fedha hizo zimepatikana
kutokana na watazamaji 32,614 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa
kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh.
30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo
ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh.
34,557,864.41, maandalizi ya mchezo sh. 28,450,000 wakati wa gharama za
uchapaji tiketi ni sh. 8,625,641.88.
Nyingine ni bonasi kwa
timu ya Taifa Stars sh. 28,798,220.34, asilimia 15 ya uwanja sh. 18,917,141.01,
asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 25,222,854.67 na asilimia 5 ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 6,305,713.67.
Asilimia 60 ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 71,885,135.82 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,783,428.20 ambayo ni asilimia 5
kutoka kwenye mgawo wa TFF.
TENGA AWAPONGEZA WACHEZAJI, SERIKALI
Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ameipongeza wachezaji wa Taifa
Stars na benchi lao la ufundi, washabiki, mdhamini na Serikali kwa kufanikisha
ushindi wa jana.
Tenga amesema ushindi
huo umetokana na ushirikiano kutoka kwa wadau wote, na hasa wachezaji
walioonesha kiwango kikubwa kulinganisha na mechi zilizopita ikiwemo kiwango
cha kujituma uwanjani.
Amesema Serikali ni mdau
mkubwa wa mpira wa miguu katika miundombinu, usalama na idara zake mbalimbali
ikiwemo Uhamiaji ambayo imefanikisha kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa mechi hiyo
ambapo Taifa Stars iliifunga Morocco mabao 3-1.
TENGA KUFUNGUA SEMINA ELEKEZI COPA COCA COLA
Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa semina elekezi ya michuano ya Copa Coca Cola itakayofanyika kesho
(Machi 26 mwaka huu).
Semina hiyo
inayoshirikisha makatibu wakuu wa vyama vya mpira wa miguu mikoa ya Tanzania
Bara na Zanzibar itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na itafunguliwa na
Rais Tenga kuanzia saa 3 kamili asubuhi.
Washiriki wengine katika
semina hiyo itakayokuwa na watoa mada kutoka TFF na wadhamini kampuni ya Coca
Cola ni waratibu wa michuano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania
(UMISSETA).
0 comments:
Post a Comment