KAMPUNI
ya Compass Communications imewatahadharisha warembo na wanamitindo
wote nchini kutorubuniwa na genge la watu wanaotumia jina la Flaviana
Matata kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai amesema jana
kuwa kuna genge la watu wanaotumia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa
facebook ujulikano kwa jina la Flaviana Matata’s na kujipatika fedha
kiasi cha sh. 200,000 kwa jila anayejiunga kwa lengo la kutafutiwa kazi
au nafasi ya kufanya shughuli za wanamitindo nje ya nchi.
Maria
alisema kuwa watu hao huwarubuni wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi
nje ya nchi kwa mgongo wa Flaviana na mmoja wa vijana hao
amejitambulisha kama ‘kaka’ yake mwanamitindo huyo, jambo ambalo si la
kweli.
Alifafanua
kuwa baada ya kukutana na wasichana waliongia katika mtego huo, huwa
wanaawalaghai kwa njia mablimbali na baadaye kulipa kiasi hicho cha
fedha. Alisema kuwa hali hiyo imewaletea usumbufu wasichana wengi na
kujikuta wakihaha kutafuta ukweli baada ya kutapeliwa.
“Compass
Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana Matata
inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia yoyote
na ukurasa huu au watu hawa. Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe
waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia
mtu yoyote kazi ya uanamitindo popote pake,” alisema Maria.
Maria
alisema kuwa ukurasa halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa
Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata” na kwa sasa wanendelea kushirikiana
na vyombo husika kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu huo.
0 comments:
Post a Comment