Na
Mwandishi Wetu, EANA
Watu
wapatao 200 wakiwemo watafiti, wanasayansi na wapanga sera wanatarajiwa
kuhudhuria mkutano wa nne wa Afya na Sayansi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) mjini Kigali, Rwanda Machi 27-29,mwaka huu.
Kauli
mbiu ya mkutano huo wa siku tatu ni : Kipaumbele cha Kanda na
matarajio:’’Ushahidi wa kuchukua hatua katika Changamoto za Mabadiliko ya
Upatikana Fedha Duniani,Shirika Huru La Habari la Afrika Mashariki (EANA)
limeripoti.
Mtaalamu
wa Masuala ya Afya wa Benki ya Dunia,Prof. Charles Mugone na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Ulaya inayoshughulikia Masuala ya Afya (EDCTB) ni
miongoni mwa wataalamu watakaotoa hotuba za ufunguzi katika mkutano huo.
Mkutano
huo utakuwa na vipengele vinavyogawaanyika katika makundi manne ikiwa ni pamoja
na Afya ya Mama na Mtoto, Magonjwa yasiyo ya kuambukiza na msongo wa
mawazo,Uimarishaji wa Mfumo wa Afya na Ubora wa Utoaji Huduma za Afya.
‘’EAC
inafahamu umuhimu ya kuunganisha nguvu katika kuimarsiha ushirikiano wa kikanda
kwenye huduma za afya hususan katika utafiti wa masuala ya afya,’’ alisema
Katibu Mkuu wa EAC, Dr Ruchard Sezibera.
Mkutano
huo utatanguliwa na Mkutano wa Pamoja wa Bodi za Wataalamu wa Afya na Mabaraza
utakaofanyika kati ya Machi 25 na 26, 2013 na Mkutano wa Tisa wa EAC waBaraza
la Sekta ya Afya.
Mikutano
ya EAC ya Afya na Sayansi huitishwa na Sekretarieti ya EAC na kufanyika ndani
ya nchi wanachama kwa mzunguko.
Mkutano
wa kwanza wa aina hiyo ulifanyika mjini Kampala, Uganda mwaka 2007,mkutano
uliofuata ulifanyika nchini Tanzania mwaka 2008 na nchini Kenya mwaka 2009.
0 comments:
Post a Comment