Meneja wa QX,Ally Abdalah(kulia) na Mpishi Mkuu
wa Bar hiyo, Emanuel Seneyo(wa pili kushoto) wakionyesha kitita cha shilingi
milioni moja baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyerembe
Munasa(kushoto) ikiwa ni mabingwa wa Safari Nyama Choma Mkoa wa Arusha
yalifanyika katika viwanja vya General Tyre mwishoni mwa wiki.Wa pili kulia ni
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja Mauzo wa Kanda,
Kitio Wilderson
Mashabiki wa Bar ya QX ya Arusha wakishangilia
na Meneja, Ally Abdalah (wa pili kulia) mara baada ya kutangazwa mabingwa wa
Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha yaliyofanyika katika viwanja vya
General Tyre mwishoni mwa wiki.
Mdau mkubwa wa QX Bar ya Arusha, Chocolate
akipata kitu roho inapenda
Hapa ni mwendo wa Nyama Choma tu, Jonson Mshana
na wenzake wakijumuika ndani ya banda la QX Bar ya Arusha,ambao ni mabingwa wa
Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha 2013.
Wzee wa Kitambi noma wakiwa katika hema la
Mabingwa wa
Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha 2013, QX
Bar ya jijini humo.
Wanahabari nao walikuwepo uwanjani hapo.
Wzee wa Kitambi noma wakiwa katika hema la
Mabingwa wa Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha 2013, QX
Bar ya jijini humo.
********
Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog Arusha
QX Pub, wametwaa ubingwa wa mashindano ya Nyama
Choma Mkoa wa Arusha, baada ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya
mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Safari Lager.
Kwa kutwaa ubingwa huo katika fainali
zilizofanyika juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa General Tyre, baa hiyo ilizawadiwa
fedha taslim Sh milioni moja pamoja na cheti.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo
mkoani hapa, Royal Stop Over Pub, walishika nafasi ya pili na kuondoka na
kitita cha Sh 800,000 na cheti, wakati Blue Line Pub walishika nafasi ya tatu
na kupata zawadi ya Sh 600,000 na cheti.
Walioibuka na nafasi ya nne ni baa ya Rombo
Delux iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya VIP Longe ilishika
nafasi ya tano na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.
Akizungumza kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji
Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote
hizo juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.
Alivitaja vigezo walivyotumia kupata mshindi
kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia
uchaguzi, uhifadhi wake na wa vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na
ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa
kwa TBL na bia ya Safari Lager kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani hapa
kabla ya kuhamia mkoa wa Moshi na wa mwisho.
“Tulianza kwa kuwataka watu wapige kura
kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa mkoa huu
wa Arusha tukapata baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo tutampata
mshindi.
“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na kula
nyama hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma
wapate nyama bora,” alisema.
Alisema kuwa bia ya Safari Lager ina miaka
takriani 36 na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo ndio inayoongoza
kwa mauzo.
Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru, NyerembeMunasa, aliisifu TBL kupitia Safari Lager kwa
kuandaa mashindano hayo, akisema kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni
hiyo katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo kama
mashindano ya Pool Safari Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao katika
michezo mbalimbali kama soka na mingineyo.
“Mashindano haya ni mazuri kwani yanawajengea
wateja wa nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii ya nyama
choma,” alisema.
Alizitaka baa ambazo hazikufika fainali,
kutokata tamaa na badala yake kujipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa
kurekebisha yale waliyokosea mwaka huu.
Chezea QX WEWE!.....Wazee wa KITAMBI NOMA
ReplyDelete