Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee` Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee
marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans (YANGA) ambaye amelezwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha kufuatia kugongwa na
BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.Mzee Mzimba
amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi. Hadi jana
hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole nyingi kwa
maumivu aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka.
*** ***
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo Jumapili Machi 10, 2013
amemtembelea Mzee Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee wa Klabu ya Dar es salaam Young
Africans (YANGA), ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini
Dar es salaam, akiuguza majeraha kadhaa kufuatia kugongwa na pikipiki maarufu
kama 'Bodaboda' wiki iliyopita katika barabara ya Nyerere.
Rais
Kikwete, ambaye amewasili leo kutokea Afrika Kusini katika ziara ya kikazi ya
siku tatu, amempa Mzee Mzimba pole na
kumuombea apate nafuu ya haraka.
Katika
ajali hiyo Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha madogo
usoni na mikononi.
Kwa
mujibu wa madaktari na wauguzi hali yake inaendelea vyema baada ya kutibiwa,
ikiwa ni pamoja na kuvishwa Plaster of Paris (Piopio).
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
10
Machi, 2013
0 comments:
Post a Comment