Nafasi Ya Matangazo

March 18, 2013



TAREHE ya leo ni ndio aliyo zaliwa Mama mzazi wa Blogger na Mpigapicha nguli Tanzania, Mroki Mroki, Bi. Mary O.Nathan  (pichani) wa Kinyenze, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye leo anatimiza miaka 60 tangu kuzaliwa kwake tarehe kama ya leo. 



Kipekee anamshukuru Mungu kwa kumjalia umri huo alionao hivi sasa. Anawashukuru wote ambao wamechangia yeye kuishi vyema. Anaishukuru sana Familia yake yote kwa umoja na upendo walio nao jambo mabalo anasema linamfanya aishi kwa furaha na amani. 



Aidha watoto wake wote wanampa Pongezi za dhati na Kumuombea Mungu amjalie zaidi Afya njema, akimpa zawadi ya Hekima na Busara katika kipindi hiki cha maisha yake ya utu uzima ambao Busara yake na Hekima vinahitajika sana ndani ya Familia yake na Jamii kwa ujumla.



Wajukuu zako na Vitukuu wako pia wanakusalimia sana na wanakuimbia kale kawimbo ka Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!!

Happy Birthday Bibi!!! Dear Bibi Happy birthday to youuuuuuuu!!!!



Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kipera , Kitongoji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakutakia heri na fanaka.



HAPPY BIRTHDAY MAMA TUNAKUPENDA SANA NA TUNAJIVUNIA KUWA NA MAMA WA NAMNA YAKO, MUNGU AKUJALIE HEKIMA NA BUSARA ZAIDI KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.



BY: FAMILIA YAKO.
Posted by MROKI On Monday, March 18, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo