Mwandishi
wetu
VIONGOZI
wa mataifa mbalimbali duniani, kila mara wanakutana katika vikao vya kimataifa
kusaka amani, bila amani hakuna kitu chochote kinachoweza kufanya nchi isonge
mbele.
Utasongaje
mbele wakati kila saa ni migogoro na vita? Lakini Watanzania tumejaliwa kwa
kiasi kikubwa kuwa na amani, ambayo kwa sasa kuna baadhi ya watu wanataka
kuichezea. Ni kama vile wamechoka nayo.
Lakini
wakati kukiwa na migogoro mingine ambayo haina tija, kuna kitu ambacho
kimeanzishwa ili kuwakumbusha Watanzania kuhusu misingi halisi tuliyowekewa na
waasisi wa Taifa hili.
Hiki si
kingine isipokuwa ni mbio za Uhuru Marathon, ambazo zitafanyika mwishoni mwa
mwaka huu huku Rais Jakaya Kikwete kwa kuona umuhimu wake naye ameamua
kushiriki kama kinara na jemedari wa Taifa hili ambapo mara kwa mara amekuwa
akiwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wa kuenzi amani iliyopo.
Akithibitisha
hilo, Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck, anasema lengo la mbio hizo ni
kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa kukumbuka, kuzingatia na kuuenzi urithi
waliaochiwa na viongozi waliopigania uhuru wa nchi.
Anasema
urithi huo ambao utakuwa ukikumbukwa kila mwaka kupitia mbio hizo, ni upendo,
mshikamano, umoja na amani iliyopo. Melleck anasema mbio hizo zitakuwa
zikifanyika kila mwaka na zitaanza rasmi siku ya tarehe 08/12/2013 na
zitatanguliwa na shamrashamra za kanda zote za Nchi yetu.
Hilo
lilithibitishwa pia na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.
Fenella Mukangara , ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati zinazinduliwa jijini Dar
es Salaam.
Uzinduzi
wa mbio hizo ulienda sambamba na kuzinduliwa rasmi kwa mtandao wa Uhuru
Marathon ambao utakuwa na habari za kila aina kuhusu mbio hizo na washirika
wake.
Dk.
Mukangara alipongeza wazo la kuanzishwa mbio hizo ambazo zitakuwa zikifanyika
kila mwaka, lengo likiwa ni kudumisha umoja, amani na upendo miongoni mwa
Watanzania na kuuenzi uhuru wetu.
Waziri
alikiri, kwa sasa kuna mbio nyingi za marathon hapa nchini, lakini hakuna ambaye
alikuja na wazo zuri la kuanzisha mbio kama hizo za kuuenzi uhuru wetu na
kudumisha amani nchini.
“Nawapongeza
waandaaji wa mbio hizi ambao ni vijana wa Kitanzania waliokuja na wazo hili
zuri la kuanzisha mbio za uhuru. Tunazo mbio nyingi sana hapa nyumbani, lakini
hatukuwa tumewaza kuanzisha mbio zinazolenga kuuenzi uhuru wetu na kudumisha
amani yetu.
“… Kwa
niaba ya Serikali, napenda kusema wazi kuwa tumefurahishwa sana na wazo hili la
kuanzisha mbio hizi za Uhuru na nichukue fursa hii kuwaomba wadau na wapenda
maendeleo ya michezo kuungana na taasisi hii kufanikisha mpango huu ili uweze
kuwa na mafanikio.
“Serikali
bado itaendelea kuweka miongozo na mazingira rafiki ya kushirikiana na wadau
wenye nia nzuri ya kuendeleza michezo nchini. Nina hakika waheshimiwa mawaziri,
wabunge, viongozi mbalimbali wa Serikali, mashirika binafsi na viongozi wa dini
wote watajitokeza kushiriki mbio hizi,” alisema.
Hapa ndipo
tunapoweza kusema kwamba, fikiria mbio zozote kubwa duniani kama vile London
Marathon nchini Uingereza, Paris Marathon, Ufaransa au zile zingine zenye
kupendwa na wengi zaidi duniani za Berlin Marathon zinazofanyika Ujerumani kila
mwaka, lakini Uhuru Marathon ni zaidi ya mbio.
Kwani mashindano
yote haya ni ya kutukuka, kutokana na kushirikisha wanariadha wenye majina
makubwa duniani, huku kukiwa na ushindani mkubwa zaidi miongoni mwa washiriki.
Lakini kwa
sasa Tanzania ina cha kujivunia zaidi kwa ujio wa mashindano ya mbio Uhuru
Marathon.
Upekee wa
shindano hilo la Uhuru Marathon ni kutokana na aina ya washiriki wake, pamoja
na kupewa tafu kubwa na waandaaji wa mashindano ya Berlin Marathon, ambao
wanataka kuiona Tanzania inatangazwa zaidi.
Hivyo,
shindano la Uhuru Marathon, lina nafasi kubwa ya kuwabeba Watanzania kwa
kutangazika zaidi, hasa ukichukulia uzoefu mkubwa walionao waandaaji wa Berlin
Marathon ikiwa pamoja na kuchangia kudumisha amani na upendo nchini.
Mratibu wa
mbio hizo, Innocent melleck anasema, ana imani mbio hizo zitajizolea umaarufu
mkubwa, kutokana na jinsi zitakavyoteka hisia za watu mbalimbali, wakiwemo
wanamichezo.
Katika
mbio hizo, zitakazowashirikisha watu wa kada mbalimbali, zitakuwepo pia mbio za
kilomita 3, kilomita 5, Half Marathon kilomita 21 pamoja na Full Marathon
yenyewe kilomita 42.
Mratibu
huyo anasema mbio za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa kada
mbalimbali, wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia zitakuwa za
kuchangia kwa ajili ya watu wa mahitaji ya aina mbalimbali.
“Hapa
tunachotaka kufanya katika mbio za kilomita 3 ni kuwaomba kama vile viongozi
maarufu wa dini mbalimbali pamoja na viongozi wetu ili kushiriki, kwa kudumisha
amani na upendo.
“Pia
tutahakikisha kama mbio za kilomita 5, zinakuwa kwa ajili ya kuchangia watu
wenye mahitaji mbalimbali na tayari tuna uhakika mkubwa wa wanariadha maarufu
zaidi duniani kushiriki,” anasema.
Mratibu
huyo anafafanua kuwa wamejipanga mno katika hilo ili kuhakikisha wanafanya
mambo makubwa zaidi na ambayo yataleta tija kwa taifa.
Wakati
Uhuru Marathon ikitambulishwa bungeni, kiongozi aliyeonekana kufurahishwa zaidi
na hilo ni Spika Anne Makinda, ambaye hakuishia kulimwagia sifa tu, bali
alitaka hata viongozi wahakikishe wanalifanikisha.
“Ni wazo
zuri hasa katika kipindi hiki ambacho tunapigania amani na mshikamano miongoni
mwetu, tunatakiwa kuenzi mashindano kama haya ili kutufanya tuwe wamoja zaidi,”
alisema Spika Makinda.
Msaada wa
Berlin Marathon
Melleck
anasema, wamefanya mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya Berlin Marathon,
kwani hilo ni moja kati ya mashindano makubwa zaidi duniani, likiwa
linashirikisha washiriki mbalimbali walio maarufu zaidi.
Shindano
la Berlin Marathon au maarufu zaidi kwa jina la BMW Berlin Marathon kutokana na
kudhaminiwa na kampuni ya BMW ni maarufu zaidi ndani ya Ujerumani na duniani
kwa ujumla.
Shindano
hilo la Full Marathon la kiilomita 42.195 ambalo linawashirikisha wanariadha wa
kulipwa na wale wa ridhaa, lilianza kwa mara ya kwanza mwaka 1974 na
linafanyika kila wiki ya mwisho wa Septemba kila mwaka.
Shindano
hili kwa umaarufu wake, mwaka 2008 lilishirikisha wanariadha takriban 40,827
kutoka mataifa 107, huku waliomaliza mbio wakiwa 35,913 na lina zawadi
mbalimbali za kuvutia.
Uhuru
Marathon je?
Melleck
anasema, ushirikiano wa Berlin Marathon una maana kubwa, kwani itasaidia
kuitangaza zaidi Tanzania na kuifanya dunia itambue umuhimu wa amani, upendo,
umoja na mshikamano miongoni mwetu.
“Wanariadha
wengi watashiriki katika mbio hizi, wengi wakiwa maarufu zaidi duniani, pamoja
na viongozi wa kada mbalimbali na hivyo kutimiza lengo tulilojiwekea.”
Mratibu
huyo anasema, kuna kila haja kwa Watanzania, kuyathamini mashindano hayo, kwani
yana lengo la kuwafanya wawe wamoja zaidi, hasa katika kipindi hiki kigumu
ambacho kuna majaribu ya kila aina.
“Waasisi
wetu wa taifa na wale waliopigania uhuru, walikuwa na malengo mengi na
tunatakiwa kuyadumisha hayo, hilo ndilo Uhuru Marathon inalotakapigania,”
anasema.
Kwa
Watanzania itakuwa faraja zaidi, hasa ukichukulia jinsi taifa linavyoweza
kufaidika kwa kuzalisha pia wanariadha wa aina mbalimbali.
Hivyo
Uhuru Marathon ni zaidi yambio, kwani inatukumbusha tulipotoka, tulipo na
tunapokwenda!
0 comments:
Post a Comment