Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bw. Wilman Kipenjama
Ndile(kulia) akipokea msaada unga na
simenti kutoka kampuni ya Ophir Energy Plc vyote vikiwa na thamani ya Sh Mil 13
wa ajili ya waahanga wa mafuriko
wilayani humo. Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw Fidelis
Lekule(kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw Wilman Kipenjam
Ndile akitoa shukrani kwa kampuni ya Ophir Energy plc mara baada ya kupokea
msaada wa chakula na saruji vypte vikiwa na thamani ya Sh Mil 13.2, kwa ajili
ya wahanga wa mafuriko wilayani humo.Wengine pichani ni Meneja Uhusiano wa
Kampuni hiyo Bw Fidelis Lekule(kushoto) na mwakilishi wa wahanga hao mlemavu wa
macho Bw Mohammed Omari.
**** *****
Na
Mwandishi Wetu,Mtwara
KAMPUNI
ya kimataifa ya utafiti wa mafuta na gesi nchini Tanzania, yenye visima uwepo
mkubwa mkoani Mtwara, Ophir Energy plc jana imekabidhi msaada wa sembe na
saruji vyenye thamani ya Sh Mil 13.2m, kwa ajili ya wahanga wa mafuriko
yaliyoikumba wilaya hiyo hivi karibuni.
Akikabidhi
msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Meneja wa Uhusiano Fidelis Lekule
alisema kampuni ayke imeguswa na janga lililowapata wana-Mtwara ndiyo maana wameamua
kutoa msaada huo.
“Ukweli
ni kwamba Ophir Energy inafanya kazi Mtwara pamoja na sehemu nyingine duniani,
hivyo matatizo na mafanikio ya wilaya hii yanaigusa kampuni kwa namna moja au
nyingine,” alisema Bw Lekule.
Kwa
mujibu wa Lekule, msaada huo unajumuisha magunia 280 ya unga wa sembe ili
kuwapa chakula wahanga hao wa mafuriko ambao chakula chao kilisombwa na maji ya
mvua na pia mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kukarabati miundombinu
iliyoharibiwa ikiwa ni pamoja na makalivati na mfumo wa mifereji ya maji katika
manispaa hiyo.
Akipokea
msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Kapenjama Ndile, aliishukuru
kampuni ya Ophir Energy kwa msaada huo na kusema umekuja wakati muafaka ili
kusaidia wananchi wenye shida wilayani Mtwara.
Akizungumzia
ukubwa wa tatizo, Mkuu wa Wilaya alisema kuwa mafuriko hayo kumbukumbu
zinaonyesha kuwa hayajawahi kutokea Mtwara katika miaka 30 iliyopita,
yalisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katikati ya Januari mwaka huu.
Alisema:
“Takwimu zinaonyesha kuwa mafuriko hayo yaliathiri zaidi ya watu 7,000, nyumba
210 zilibomolewa na zingine 385 ziliharibiwa kwa njia moja au nyingine.
Ndile
alisema kuwa ofisi yake iko mbioni kutengeneza vyeti vya shukrani vitavyotumika
kuwatambua watu waliojitokeza kusaidia wananchi wa Mtwara ikiwa ni pamoja na
kampuni ya Ophir, wakati wa kipindi hicho cha matatizo.
Mkazi
mmoja wa Mtwara mwenye ulemavu wa kutoona ambaye aliwawakilisha wahanga wengine
wa mafuriko hayo katika hafla hiyo fupi ya kupokea msaada, Mohammed Omari,
alishukuru kampni ya Ophir kwa msaada huo ambao umekuja katika kipindi muafaka
na kupitia ofisi ya Mkuu wa Wilaya, “Nyumba yangu ilikumbwa na mafuriko.
Chakula
changu na mali zingine za thamani
zilizokuwemo ndani ya nyumba viliharibiwa kabisa,” alilalamika mlemavu
huyo kwa masikitiko makubwa.
0 comments:
Post a Comment