MELI
ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC)
imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo
wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo
kwenye Meli hiyo. Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua
tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho
ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini
majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika
eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa
toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao hawakutoa ushirikiano
kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa wakati wakilaumiana
zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea katika moja
ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto zilipopenya na
kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.
Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja
na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba
Mkoani Kagera leo usiku.
Maafisa
wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo
mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa
tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa
katika chumba cha kuhifadhia mizigo.Picha/ Habari Na Gsengo Blog Kwa Picha Zaidi Mtembelee Kwa Kubofya Hapa
0 comments:
Post a Comment