Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu (Hayat-ulamaa) Shk. Suleiman Amran Kilemile Akitoa Nasaha Juu ya Umuhimu wa Waislam Kiimarisha utekelezaji wa Ibada ya Kutoa Zakat kwa Makundi yaliyotaja Katika Qur'an kwani ndio Njia rahisi ya Kuimarisha Uchumi wa Jamii na Nchi kwa Ujumla.
Kijana Mfanyabiashara Ndogo Ndogo Ambae amekuwa akitoa Zakat mara kwa Mara akitoa ushuhuda jinsi gani utoaji wa Zakat Umemsaidia kulinda na Kukuza Biashara yake katika Mkutano wa Ugawaji Zakat.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baytul -ulmaal (Charity Fund) Tanzania akisisitiza Umuhimu wa Matajiri na Wasomi wa Kiislam Kushiriki Kikamilifu kuimarisha Mfuko huo kwa Maslahi ya Ustawa wa Jamii hasa Masikini na wenye mahitaji maalum ili kuleta uiano wa kimaendeleo.
Baadhi akina Mama wakifuatilia kwa Makini Mada Juu ya Utekelezaji wa Ibada ya Zakat ambayo ni Nguzo Muhimu katika dini ya Kiislam yenye lengo la kupambana na Umasikini ndani ya Jamii ya eneo husika.
Kijana Mwanafunzi Yatima anayejiunga na Shule ya Serikali Akipokea Tshs 100,000 Kutoka kwa Sheikh Suleiman Kilemile kama Fungu la Zakat lililotolewa Katika Ukumbi wa Lamada Ilala. Mfuko wa Baytul –ul maal Unaendeshwa pamoja kati ya Wanataalum wa fani mbali mbali za kimazingira pamoja na Wanazuoni wa Kiislam kukuzanya Zakat pamoja na Waqfu kwa manufaa ya Jamii ya Kiislam.
. Waumini wa Kiislam wakimsikiliza Shk Twaha Bane wakati akieleza Umuhimu wa Waislam kuitekeleza Nguzo ya Zakat kwani inaleta Upendo, Amani na Uimara wa Biashara kwa Mtoaji na Anayepokea.
0 comments:
Post a Comment