Meneja wa kinywaji cha castle lite Pamela kikuli akimpongeza mshindi wa shindano laFeel the Beet of Sub Zero’ nchini Afrika ya kusini , Caroline Lupilli lililoendeshwa kwa kuwashirikisha washiriki wa mtandao wa facebook
***
WATANZANIA watatu waliobahatika kuhudhuria tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama ‘Feel the Beet of Sub Zero’ wamejulikana.
Tamasha
hilo la kimataifa linaloandaliwa na kinywaji cha Castle Lite,
linatarajiwa kufanyika Johannesburg, Afrika Kusini Februari 2, mwaka
huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya
Castle Lite inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Pamela
Kikuli, alisema watu hao watalipiwa kila kitu ikiwa pamoja na nauli ya
kwenda na wenza wao watakaowachagua.
Pamela
aliwataja watu hao ambao walipatikana kupitia shindano lilikuwa
likiendeshwa katika kurasa ya Castle Lite kwenye mtandao wa kijamii wa
Facebook, kuwa ni Caroline, Edger na Eric.
“Hii
ina maana kuwa Castle Lite itawalipia watu sita ikiwa ni gharama za
kwenda huko, kwani tulisema kila mmoja ataenda na rafiki yake
atakayemchagua.
“Tumefanya hivi ikiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii, maana kwa kiasi kikubwa imetuunga mkono katika mambo mbalimbali,” alisema.
Mwanamuziki maarufu atakayetumbuiza katika tamasha hilo ni Kanye
0 comments:
Post a Comment