Nafasi Ya Matangazo

January 21, 2013


Baadhi ya nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya jikoni
Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula akiangalia nyumba ya shirika hilo kabla ya kuikabidhi kwa mnunuzi wa nyumba hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
Mmeona mandhari ya nyumba ilivyokuwa nzuri
Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula (kulia) akimkabidhi funguo ya nyumba, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
Wakipewa kadi ya Luku
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid akiweka saini baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid. Kulia ni Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula.  
Karibuni ndani
Posted by MROKI On Monday, January 21, 2013 1 comment

1 comment:

  1. AnonymousJuly 29, 2022

    Napenda kujua utaratibu wa kupata hizo nyumba hasa kwa wanachama

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo