NINANI
amekwambia etyi ukiwa na noti chakavu ndo hupati huduma? Hiyo labda ni huko
kwenu mnao jidai mnaijua hela lakini si Mkoani Kigoma ambako wanaitafuta fedha
na kuitumia hadi Benki wenyewe waseme sasa inatosha.
Kigoma ni
watumiaji wa zuri sana wa fedha. Hili ni kutokana na namna wanavyotumia noti za
thamani mbalimbali ya malipo kuanzia ile ya shilingi 500-10,000 ambazo wakati
mwingine huwa chakavu kiasi cha kutisha lakini wao bado huendelea kuiweka
katika mzunguko.
Hili ni
jambo jema sana na lakuweza kuigwa kwa mikoa mingine nchini kwani Mikoa mingi
hasa jijini Dar es Salaam fedha ikiwa chafu au chakavu kama hiyo ionekanayo
pichani waweza kudoda nayo mkoni na usipate huduma.
Mkoani Kigoma
na vitongoji fedha hizo hutumika hadi pale itakapoingia mikoni mwa Benki na
ndio kuwa mwisho wa matumizi yake.
Zipo
noti chakavu zaidi ya hiyo inayoonekana pichani, lakini wala wananchi
wa Kigoma hawatii neno pindi wanapo pewa kama chenji au kutoa kupata
mahitaji.
Mtu
asiyezoea akipewa fedha hiyo anaweza kugombana na mwenye duka au mtoa huduma
yeyote mkoani Kigoma lakini ajabu ni kuwa wewe unaehoji uchakavu wa not indo wanakushangaa
maana Benki hawajasema fedha hiyo sio halali kwa malipo ya thamani husika.
0 comments:
Post a Comment