Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Nguruka
Wilayani Uvinza mkoani Kigoma leo wakati Katibu Huyo na Wajumbe wengine wa
Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi walipotembelea Kijiji hicho na kufanya
mkutano na wakazi wa eneo hilo baada ya kuhudhuria kikao cha ndani cha Siasa
Kata ya Nguruka. Wajumbe hao walipata mapokezi makubwa Kijijini hapo.
Katibu wa
Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akicheza na mmoja wa
akina mama wa Kijiji cha Nguruka ambaye alifurahi sana baada ya kumuona ‘live’
Naibu Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN).
Katibu wa
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa katika msafara wa mapokezi ya Sekretarieti
ya Chama cha Mapinduzi huku akipiga ngoma kwa umahiri mkubwa na kuwafurahisha
wengi. Kulia ni Mjumbe wa NEC, Asha Baraka.
Wananchi wa Nguruka wakiwa kando ya barabara kusubiri
Msafara wa Sekretarieti ya CCM.
Katibu wa
Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) akiwa na Mjumbe
wa NEC kutoka Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Asha Baraka ambaye ni mzaliwa wa
Nguruka mkoani humo wakati wa mapokezi ya wajumbe hao wa Sekretarieti.
Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro akisalimia wananchi wa Nguruka.
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifanya vitu
vyake.
Vijana hawa walikuwa njiani tayari kwa kutoa maelekezo wapi
pa kupita.
Msanii Umy Wenceslaus maarufu Dokii ambaye amekuwa ni Kada
maarufu wa Chama cha Mapinduzi akitoa burudani kwa wakazi wa Nguruka hii leo.
Dokii pia alitoa burudani katika mkutano Kijiji cha Uvinza.
0 comments:
Post a Comment