Msanii
wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’ akitoka
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, licha ya dhamana yake kuwa wazi,
lakini alishindwa kutoka kwasababu ya kukosekana kwa Msajili wa Mahakama
Kuu. Msanii huyo sasa atatoka kesho baada ya kurudishwa tena mahakamani
kwa ajili ya kuangalia kama ametimiza masharti ya dhamana yake.
Pamoja
na hayo, mwonekano wa msanii huyo unazidi kutia wasiwasi. Handeni Kwetu
ilipokea simu nyingi zinazotaka kujua kama kweli mwanadada huyo ni
mjamzito. Hata hivyo, wataalamu wa mambo wanaweza kuchunguza vyema
wakati na sisi tunasubiri kupata kauli yake au vipimo vya daktari.
Lulu akipanda gari lililomleta Mahakamani.
0 comments:
Post a Comment