Pombe ya asili ya kabila la wafipa inayotengenezwa kwa ulezi na kunyewa kwa mirija, raha duniani.
Mama
Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
akiwasili katika ukumbi wa St. Maurus Chemchem Mjini Sumbawanga jana
katika sherehe aliyoalikwa na Mkuu wa Mkoa Rukwa Injinia Stella Manyanya
ya kuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka 2013 iliyoenda sambamba na
tamasha kubwa la mwanamke wa Rukwa RUWA (Rukwa Women in Actiion).
Tamasha
hilo lililobuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa lina lengo la kuwanunganisha
wanawake wa Mkoa wa Rukwa pamoja katika tamaduni zao tofauti katika
kuwainua kiuchumi na kifikra ambapo walishiriki kwa kuonyesha tamaduni
zao za ngoma, mavazi na chakula. Lengo la tamasha hilo pamoja na umoja
huo ni kwa ajili ya kunadi na kuhamasisha utalii wa ndani, kuwawezesha
kinamama wa kipato cha chini, kuhamasisha na kuwezesha vita dhidi ya
umaskini, mimba za mashuleni, lishe bora na chanjo za afya kwa watoto
wachanga na wanawake wa kipato cha juu kuwawezesha wa kipato cha chini.
Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake katika tamasha hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika tamasha hilo
kumkaribisha mke wa Waziri kuzungumza na washiriki zaidi ya mia sita
walihudhuria katika tamasha hilo.
Mama
Pinda (kulia), Mama Dora Rajab Rutengwe mke wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi
(wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya na wanawake
wengine wakijumuika kucheza muziki wa kwaito katika kupasha misuli moto
kwenye tamasha hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akionyesha vazi linalotangaza
utalii wa ndani na rasilimali muhimu kama misitu, wanyama pori, na
samaki.
Ilifika muda washiriki wa maonyesho hayo kupita mbele ya jukwaa kuu tayari kwa kuanza kuonyesha sanaa na mitindo mbalimbali.
Mmoja ya washiriki akionyesha moja ya vazi la kiutamaduni la asili ya makabila ya Rukwa kwa wazee wakati wa msimu wa baridi.
Katibu
tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisakata ngoma ya
kinyaturu katika tamasha hilo. Kulia ni mwanae Hussein Chima.
Mama
Tatu Chima mke wa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa akimpa zawadi ya shanga za
kabila la kinyaturu Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Tunu Pinda kabla ya kuanza kucheza ngoma ya kabila hilo.
Kulia ni mumewe Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa (wa pili kushoto) Injinia Stella Manyanya akishiriki
kwenye ngoma ya kabila lake la wangoni waliojumuika kwenye tamasha hilo
kuonyesha baadhi ya tamaduni zao. Wa kwanza kushoto akionyesha uwezo
mkubwa katika kusakata ngoma hiyo ni mwandishi wa habari wa channel ten
Judy Ngonyani.
Mduara pia umo katika ngoma za kabila la wangoni.
Washiriki wa kabila la wahaya wakionyesha baadhi ya mavazi ya asili ya kabila lao.
Ngoma za kihaya.
Majaji
waliohusika katika katika mashindano ya tamaduni za makabila tofauti ya
Mkoani Rukwa, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Kagera, Singida, Kigoma, Shinyanga
na Mwanza. Mkoa wa Rukwa ulishinda katika Ngoma.
Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha baadhi ya mavazi yao ya asili na baadhi ya zana zao za asili.
Sound
ya ngoma ya kabila la wafipa ikitumbuiza katika tamasha hilo. Kigoda
hutumika kusugua chungu ambacho hutoa mlio wa aina yake katika kunogeza
ngoma ya kabila hilo.
Washiriki wa kabila la wafipa wakionyesha tamaduni zao za kusaga unga na ulezi kwa kutumia zana za asili.
Mambo yetu ya rusha roho nayo yalikuwepo.
Palikuwa hapatoshi.
Mvua
ya shampen ya kukarisha mwaka mpya 2013 ikifunguliwa na mratibu wa
tamasha hilo ambae pia ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Ndugu
Deonisya Njuyui.
Cheers
kwa mwaka 2013. Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu akigonganisha glass
na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Mkoa wa Rukwa Ndugu
Samson Mashalla na Mke wa aliyekuwa Mbunge jimbo la Sumbawanga Mjini
CCM Aeshi Hillal.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Idd Kimanta akinywa togwa iliyoandaliwa na kabila la wahaya.
Mbunge wa Jimbo la Kalambo Josephat Kandege nae akilamba tongwa.
Mama
Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakionja ugali wa muhogo
ulioandaliwa na kabila la Waha kutoka Kigoma.
Ndizi kuku au Kuku ndizi kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.
Maharage yaliyochanganywa na mboga za majani kutoka katika kabila la wanyakyusa la Mkoani Mbeya.
Mshiriki
Leah Mgagama kutoka katika kabila la wangoni akionysha moja ya vazi la
kabila hilo na kifaa cha kuhifadhia chakula kisiharibike kijulikanacho
kwa jina la "Kijamanda".
Vazi la kitanzania likiwa na bandera ya taifa.
Ilikuwepo mitindo mbalimbali ya mavazi.
Onyesho la mavazi
Onyesho ya vazi la mjamzito.
Anthonia Nkyabonaki kutoka kabila la wahaya akionyesha mtindo wa mavazi. (Picha na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa- rukwareview.blogspot.com)
NIKUTAKIE MWAKA MPYA (2013) MWEMA WENYE MAFANIKIO TELE.
0 comments:
Post a Comment