Heka heka langoni mwa Yanga... Mlinda Mlango wa Yanga, Said Mohamed akijaribu kuokoa hatari hiyo langoni kwake.
Na Mwandishi Wetu
KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest Brandts
amesema timmu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi
ya Black Leopards ya Afrika Kusini niliyopangwa kufanyika kesho (Jumatano) mjini
Mwanza.
Brandts alisema wachezaji wake wote wamefikia
kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa
mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara.
Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na
walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja
waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.
“Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo
kikubwa kabla ya kuanza kwa LigiKuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango
vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza
hawatayafanya tena,” alisema Brandts.
Kuhusiana na mabacha wawili, Mbuyu Twite na
Kabanga Twite kucheza upande wa kulia, Brandts alisema kuwa wachezaji hao
wana uwezo wa kucheza nafasi nyingi katika timu yake na uamuzi huo ulikuwa na
faida kwa Yanga.
“Kabanga anauwezo wa kucheza nafasi ya
ushambuliaji, katikati, beki zote na hata Mbuyu ana uwezo huo, hivyo uwepo wao
katika timu ni mkubwa, niliwapumzisha kutokana na mipango ya mechi na wala si
vinginevyo,” alisema.
Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto alisema
jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara,
pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa Mwanza.
Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi
yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwapa
waonyesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.
“Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya
Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa
ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa
pili,” alisema Kizuguto.
0 comments:
Post a Comment