Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Elias Mtandu (Kushoto),
akiwa pamoja na Meya wa manispaa ya Morogoro Amir Nondo (Kulia) na Mratibu wa
mradi wa afya ya mama na mtoto wa Aga Khana Sisawo Konteh (Kushoto) ,
wakinyanyua mikono ikiwa ni ishara ya kushikana mikono pamoja katika kuunga mpango wa huduma bora ya Afya
ya mama na Mtoto kwa Mkoa wa Morogoro.
*****
Kituo
cha Huduma za Afya cha AKHS kimezindua mradi ambao utachangia kuboresha huduma
ya afya ya mama mjamzito na mtoto nchini Tanzania uzinduzi uliofanyika
mkoani morogoro.
Mradi
huo unaojulikana kama Tushikane Mikono Kuboresha huduma kwa Wajawazito, na Afya
ya Mtoto (Joining Hands: Improving Maternal, Newborn and Child Health (JHI),
umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Canada (CIDA) kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania.
Mradi
huo wa JHI ni kulingana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs 4 na 5, ambao
umelenga kuchangia kuboresha uzazi kwa wajawazito na watoto wachanga, (MNCH)
katika mikoa mitano ya Tanzania.
Mradi
huo utatekelezwa kupitia Kituo cha Huduma ya Afya cha Aga Khan nchini Tanzania
(AKHST) na vituo vyake vitano vya afya ya awali (PMCs) kwenye mikoa ya Dodoma,
Mwanza, Mbeya, Iringa, na Morogoro ikiwa na lengo la kujenga uwezo wa huduma za
Afya kwa jamii na kuimaimarisha uhusiano na huduma ngazi ya rufaa.
Aidha,
Mradio huo wa JHI unajivunia Shirika la Kimataifa la CIDA juu ya uwekezaji
mkubwa nchini Tanzania na mtazamo wake juu ya nia yake ya kipaumbele kwenye
sekta ya afya nchini.
Mradi
huo pia utatumika kwa kuinua uwekezaji mkubwa uliofanywa na CIDA pamoja na
serikali katika kutekeleza mikakati yake.
Malengo
ya mradi huo wa JHI ni pamoja na: kuboresha ubora wa huduma kwa wajawazito,
Afya ya Mtoto na kulenga kuongeza uwezo wa maeneo ya mradi; kuongeza
upatikanaji na matumizi ya huduma za Wajawazito, Watoto na Afya ya Mtoto na
kulenga watu wa kipato cha chini na makundi ya wakazi maskini, na hasa katika
kuongeza uwezo wao wa kupata nafuu wa kupata huduma, ubora wa huduma za Afya ya
uzazi na Wajawazito, Watoto na huduma ya Afya kwa mtoto katika ngazi ya kwanza
ya vituo vya Afya; na kuboresha njia za afya, usafi na lishe ya familia kwa
walengwa husika (MNCH) kuongeza mahitaji ya huduma (MNCH) ubora kwa walengwa;
na kuongeza maarifa uhamisho na kubadilishana juu ya masuala muhimu katika
Ushirikiano MNCH Umma muktadha (PPP).
Mradi
wa JHI wa kuboresha Afya ya mama na mtoto ulizinduliwa Julai 2012 nchini
Tanzania na unatarajiwa kuendelea hadi mwaka 2015
0 comments:
Post a Comment