Mwanamuziki
nguli wa Kimataifa kutoka nchini DRC-Congo JB Mpiana akiimba jukwaani
mbele ya mashabiki kiduchu (hawapo pichani) usiku wa kuamkia leo kwenye
viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo kiingilio kilipangwa
kuwa ni sh 25,000/= kwa laki moja wale wa VIP.
*********
BENDI ya Wenge BCBG usiku wa
kuamkia janao ilikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliofika kwenye
viwanja vya Leaders Club kushuhudia uzinduzi wa albam ya pili ya Bendi ya
Mashujaa ya Risasi Kidole, huku matatizo ya kiufundi yakisababisha bendi ya
Mashujaa kushindwa kuzindua albamu hiyo.
Pamoja na kuchelewa kuanza kwa
shoo hiyo, kutokana na matatizo ya kukatika kwa umeme kila muda, JB Mpiana
alianza kuwatanguliza wanamuziki wake wakiongozwa na mmoja wa waanzilishi wa
bendi hiyo, Shai Ngenge, na kupiga sebene kabambe kabla ya kufuatiwa na wimbo
wa zamani wa Kinie Bouger, ambao enzi zake alishirikiana
na akina, Ngiana Makanda, miaka ya katikati ya 1990.
Wimbo huo uliweza kuondoa kero
kwa mashabiki hao na kuwasahaulisha yale yaliyokuwa yakiwatokea wanamuziki wa
Mashujaa, ambao kila walipokuwa wakipanda jukwaani na wanapofika kuanza sebene
umeme unakatika, jambo lililowafanya kupanda jukwaani mara nne, lakini
wakishindwa kumaliza wibo mmoja tu wa Risasi Kidole.
JB Mpiana alionekana kuwa ni
mkombozi kwa mashabiki wachache waliokuwa wamebaki huku wakipiga moyo konde
kuwa hawataondoka viwanjani hapo bila ya kumuona JB, katika uzinduzi huo
kutokana na burudani safi.
Kitu ambacho kiliwashangaza
mashabiki wengi ni kutokatika kwa mara kwa mara kwa umeme kama ilivyotokea kwa
bendi ya Mashujaa ilipokuwa jukwaani. Mpiana aliweza kufanya kweli
katika shoo hiyo kwani umeme haukukatika mpaka aliposhuka jukwaani majira ya
saa 10 alfajiri.
Katika shoo hiyo, Mpiana
aliweza kupiga nyimbo mbali mbali za zamani ikiwa pamoja na Barakuda, Djodjo
Ngonda, Walay Danico, Dizo Dizo na zile mpya katika mtindo wa non-stop.
Mashujaa ndio walikuwa wa
kwanza kupanda jukwaani na mara walipoanza kucheza shoo ya ufunguzi ambao
imewajumuisha wanenguaji wa kike na wa kiume na waimbaji, umeme ulikatika na
kazi ya kuanza kurejesha ikaanza na kuchukua muda wa dakika zisizopungua 30.
Tatizo hilo liliendelea mara
kwa mara huku bendi hiyo ilishindwa kumaliza tatizo hilo na jitihada za kutatua
hazikutoa jibu la mara moja, huku Mmoja wa viongozi wa Bendi hiyo, King Dodoo,
akionekana kuhaha kila kona ya uwanja huo akiwa na Babu aliyekuwa akijitahidi
kusoma dua ili Jenereta hilo liweze kufanya kazi bila kusumbua.
Mafundi walijitahidi
sana na mara baada ya mashabiki kutaka JB Mpiana apande, mafundi walitatua
tatizo hilo na kumwezesha mwanamuziki huyo kufanya shoo bila tatizo hadi
alipomaliza ratiba yake.
Katika tukio jingine
lililojitokeza viwanjani hapo ni Mkurugenzi wa bendi hiyo, Mama Sakina,
aliyeanguka ghafla, ikieleza ni presha ya ghafla kutokana na kile kilchokuwa
kikiendelea mahala hapo na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Uongozi wa bendi ya Mashujaa
ulisema kuwa watafanya uzinduzi mwingine katika tarehe ambayo itatangazwa hapo
baadaye.
Baadhi
ya Wadau na mafundi wakiwa wamelizunguka Jenereta walipokuwa
wakishindwa kubaini tatizo liko wapi kutokana na hitilafu zake za mara
kwa mara.
Mashabiki wakiserebuka hivyo hivyo mara JB Mpiana na kundi lake la Wenge BCBG walipopanda jukwaani.
Baadhi ya Wanamuziki wa JB Mpiana wakitumbuiza jukwaani
Baadhi
ya wanamuziki wa bendi ya Mashujaa wakiongozwa na Chalz Baba
wakitumbuiza jukwaani,kufuatia tatizo/hitilafu ya umeme bendi hiyo
ilishindwa kuzinduza albamu yake ya Kidole Risasi.
Mdau Ben Kinyaia kutoka Clouds TV akiruka Live kunasa matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
Wadau waliofika kwenye uzinduzi wa albamu ya pili ya Mashujaa band
Charls Bakishuka kutoka katika trekta alilo wasili nalo viwanja vya Leaders katika uzinduzi wa album yao ya pili.
Pichani juu na chini ni madansa wa bendi ya Mashujaa wakitumbuiza jukwaani.
0 comments:
Post a Comment