Nafasi Ya Matangazo

December 03, 2012

Timu za Soka za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazoshiriki michuano ya mwaka huu ya Tusker Cecafa Challenge huko Uganda zimetimnga nusu fainali za michuano hiyo baa da ya kuzitoa mashindano timu za Rwanda na Burundi. 

Wawakilishi hao ni Tanzania bara Kilimanjaro Stars na Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ zimefuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya Tusker Challenge Cup baada ya kuwatoa vigogo hao katika hatua ya Robo fainali.

Kwa matokeo hayo ya timu hizo ambazo Kilimanjaro Stars iliibwaga Rwanda 2-0 katika robo fainali ya kwanza na Zanzibar Heroes ikaitoa Burundi kwa mikwaju ya Peanti 6-5 zinaweza kukutana katika fainali endapo zitafanikiwa kuwatoa washindi wa michezo ya kesho. 

Robo fainali za kesho zitawakutanisha Kenya na Malawi na mchezo mwingine ni kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia.  

Wachezaji wa timu ya Zanzibar Heroes na Burundi wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya pili ya michuano ya Tusker Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda leo.

Kiungo mchezeshaji wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Mwinyi Kazimoto akizuiwa na beki wa Rwanda, Ismail Nshutiyamagara wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michuano ya Tusker Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda leo.

Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichopambana na Burundi katika mchezo wa Robo Fainali ya Pili ya michuano ya Tusker Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda leo.Kikosi hichi kimeitoa Burundi kwa magoli 6-5.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Amri Kiemba na beki wa timu ya Rwanda, Michel Rusheshangoga wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Robo  Fainali ya kwanza ya Tusker Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda
Wachezaji wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakitoka Uwanjani baada ya kipindi cha kwanza kumalizika katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michuano ya Tusker Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda


Kipa wa Rwanda aliyelala chini akijitahidi kuokoa goli lililofungwa na Amri Kiemba baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Mwinyi Kazimoto ya kuwapita mabeki wa timu ya Rwanda
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Mrisho Ngasa aliyelala chini na wachezaji wenzake wakishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kuwafunga Rwanda 2-0 katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda
Mashabiki wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wakishangilia wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michunao ya Tusker Cecafa Challenge dhidi Rwanda uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda. Kilimanjaro Stars ilishinda 2-0
Posted by MROKI On Monday, December 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo