Shirikisho
la Mpira wa Miguu na Vilabu vya Ligi Kuu wamo katika hali ngumu mno
kifedha baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kuzuia fedha za Shirikisho
zilizoko kwenye akaunti za TFF.
Jambo
hili limesababishwa na sakata la Kodi ya “PAYE” toka kwenye mishahara
ya makocha wa timu za Taifa wanaotoka nje ya nchi. Serikali iliyoko
madarakani inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilijitolea kulipia makocha wa kigeni,
kuanzia kocha Maximo, Jan Poulsen na wengineo.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu wakiwa ndiyo wasimamizi wakuu wa mpira wa miguu hapa
nchini, ndiyo wanaongia mikataba na makocha hao, na malipo yanalipwa na
serikali moja kwa moja kwenye akaunti za makocha kupitia benki, hivyo
nijukumu la serikali kukata kodi ya “PAYE” kila inapopeleka mshahara.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania wanalidai Shirikisho la Mpira wa miguu kiasi cha
shilingi milioni 157,407,968.00 za Kitanzania, zikiwa ni kodi ya “PAYE”
kuanzia kipindi cha kocha Maximo na wengineo hadi sasa. Shirikisho la
Mpira wa Miguu linapenda kueleza kuwa uwezo wa kulipa deni hilo hatuna,
vilevile makocha wa kigeni ni msaada uliotolewa na serikali ya awamu ya
nne katika kutimiza ilani yake ya uchaguzi. Malipo kama tulivyoeleza
yanalipwa moja kwa moja serikali kwenye akaunti za makocha, hivyo suala
hili linapaswa kamalizwa na pande pili za serikali kwa maana Mamlaka ya
Mapato na Wizara yetu husika.
Kitendo
cha Mamlaka ya Mapato Tanzania kuchukua fedha za Vilabu vya Ligi Kuu
kutoka kwenye akaunti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu, fedha ambazo
zimetolewa na mdhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa Vilabu vya Ligi Kuu,
kitasababisha matatizo katika uendeshaji wa Ligi. Jambo ambalo lingeweza
kuepukika kwa pande zote kukaa chini na kujadiliana kisha kufikia
muafaka, kwani wanaoadhibiwa hapa ni vilabu. Shirikisho kwa kushirikiana
na Vilabu tupo kwenye mchakato wa kuunda kamati kwa ajili ya kuonana na
pande zote husika.
SUNDAY KAYUNI
KAIMU KATIBU MKUU
0 comments:
Post a Comment