SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu
Tanzania limeteua wadau 10 kwa ajili ya kusaidia timu ya taifa ya vijana walio
na umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys itakayopambana na Congo (Brazaville)
katika mechi ya raundi ya tatu ya michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika.
Uteuzi huo umefanywa na Rais
wa TFF, Leodegar Tenga baada ya Kamati ya Vijana ya TFF kufanya kikao chake
kujadili kwa umakini ushiriki wa timu hiyo na kupeleka mapendekezo yake kwa
rais huyo wa shirikisho.
Kutokana na umuhimu wa mechi
hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, TFF
imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo itakuwa na majukumu mawili makubwa
ambayo ni:
1. Kuhamasisha
vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo
2. Kuhamasisha
umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.
Walioteuliwa kuunda kamati
hiyo ni:
1. Ridhiwani
Kikwete Mwenyekiti
2. Ahmed
Seif (Magari) Mjumbe
3. Nassoro
Bin
Slum Mjumbe
4. Henry
Tandau Katibu
5. Ahmed
Mgoyi Mjumbe
6. Aboubakar
Bakhresa Mjumbe
7. Angetile
Osiah Mjumbe
8. Kassim
Dewji Mjumbe
9. Abdallah
Bin
Kleb Mjumbe
10. Salim
Said Mjumbe
Baada ya kuvuka raundi mbili
za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na wapinzani wake kujitoa, timu ya
Serengeti Boys inahitaji kufanya kila iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye
mashindano hayo na kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo
pia zitatoa wawakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia. Mechi za
kwanza za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za
marudiano zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012
*Kuhusu suala la Azam FC
kuwasimamisha wachezaji watatu kwa tuhuma za kuhusika kuhujumu timu, tayari TFF
imepokea barua hiyo ya Novemba 8, 2012 na inalishughulikia na kulifuatilia kwa
makini.
*TFF inapenda kukipongeza
Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Mwanza kwa kufanya uchaguzi wake kwa amani
na kufanikiwa kupata viongozi wapya watakaokuwa chini ya uenyekiti wa Jackson
Songora. Rais wa TFF amewapongeza viongozi waliorekjea madarakani na viongozi
wapya akieleza magtumaini yake kuwa kamati mpya ya Utendaji ya MRFA itaelekeza nguvu
zake katika kuendeleza mikakati iliyokuwepo ya kuinua kiwango cha mpira wa
miguu na kubuni mikakati mingine kwenye mkoa huo na Tanzania kwa ujumla
ikishirikiana na TFF.
*Ligi Kuu ya Vodacom
inatazamiwa kuendelea kesho kwenye viwanja tofauti
1. Simba v
Toto
Africans Uwanja
wa Taifa
2. T.
Prisons v
JKT
Ruvu Sokoine
3. Kagera
Sugar v
Polisi
Moro Kaitaba
4. African
Lyon v
Mtibwa
Sugar Azam
Complex
5. Oljoro
JKT v
Ruvu
Shooting Sheikh
Amri Abeid
6. Mgambo
JKT v
Azam FC Mkwakwani
Jumapili
1. Coastal
Union v Young
Africans Mkwakwani
0 comments:
Post a Comment