Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa,
wakati alipofika katika Kijiji cha Ilembo Mkoa wa Katavi, Nov 24, kwa
ajili ya kuzindua rasmi Ujenzi wa Nyumba za gharama nafuu, zinazojengwa
na Shirika hilo, ambapo jumla ya nyumba 250, zinatarajia kujengwa katika
eneo hilo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nehemiah Kyando
Mchechu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Nyumba za
Gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa, NHC katika
Kijiji cha Ilembo Mkoani Katavi. Uzinduzi huo ulifanyika Nov 24, 2012
katika kijiji hicho. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nehemiah
Kyando Mchechu (wa pili kulia) ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye na (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa
Katavi, Dkt. Rajab Lutengwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
mkewe Mama Zakhia Bilal (wa pili kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye (wa pili kulia)
wakikagua sehemu ya ujenzi wa nyumba hizo bada ya uzinduzi wa mpango wa
Ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la
Taifa NHC, katika kijiji cha Ilembo Mkoani Katavi Nov 24, 2012
0 comments:
Post a Comment