Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi taifa (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa CCM unaoendelea hivi sasa katika ukumbi wa Kizota mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume na Kulia ni Makamu Mwenyekiti Bara, Pius Msekwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akisoma taarifa ya serikali ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Wajumbe wa mkoa wa Iringa wakifuatilia kwa ukaribu taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Baadhi ya wajumbe wa mkoa wa Arusha wakiwa katika mkutano huo leo.
Baadhi ya wake wa Viongozi na waasisi wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo.
Wajumbe kutoka mkoa wa Dodoma ambao ndio mkoa wenyeji wakifuatilia kwa umakini taarifa mbalimbali za utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi kutoka nchi za Ulaya (watanzania waishio nje ya nchi) wakijilikana kama Wanadiaspora wakifuatilia mkutano huo leo mjini Dodoma. Kundi hili limekuwa mstari wa mbele katika kuwaunganisha watanzania waliopo nje ya nchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
Baadhi ya wakuu wa Wilaya mbalimbali nchini wakifuatilia mkutano huo wa nane wa chama cha Mapinduzi mjini Dodoma.
Wajumbe kutoka Manyara wakiwa mkutanoni.
Wakuu wa Wilaya wakiwa mkutano.
Wajumbe kutoka Zanzibar nao wapo.
Wakuu wa Mikoa mbali mbali nao wapo mjini Dodoma katika mkutano wa nane wa CCM.
Wajumbe wa mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba mbalimbali za taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiwa na wajumbe wenzake wa Mkoa wa Lindi.
Wajumbe wa Mkoa wa Iringa wakifuatilia kwa ukaribu matukio ndani ya mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali kutoka mkoa wa Pwani, wakiwa ndani ya ukumbi wa mikutano.
0 comments:
Post a Comment