Nafasi Ya Matangazo

November 23, 2012

 Kalusha Mbwalya  Rais wa Shirikisho la soka Zambia  FAZ, katikati ni Balozi wa Tanzania  nchini zambia  Grace Mujuma na  kulia  ni afisa balozi wa Tanzania  nchini  Zambia  Jeswald Majuva wakiwa katika picha ya pamoja.

Pichani kulia ni Rais wa Shirikisho la soka Zambia  FAZ,Kalusha Bwalya akiwa ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini humo,kwa ajili ya uthibitisho wa kutoa taarifa ya ujio wa timu ya Taifa ya Zambia Chipolo polo nchini Tanzani kwa ajili ya kucheza na timu ya Tanzani ,aidha imeelezwa kuwa timu ya Chipolo polo itainigia nchini Desemba 16  na kukaa takribani wiki nzima nchini Tanzania kwa kufanya mafunzo yao  ya maandalizi ya kwenda Afrika Kusini.Habari kwa hisani ya Mdua wa Jiachie Blog aliyeko Zambia.
========   =======  ========
Rais wa Shirikisho la Soka Zambia FAZ  Bwana Kalusha  Mbwalya  amesema Timu  ya soka ya  Taifa ya Zambia wanaafrican champion wanachipolopolo wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Taifa  ya Tanzania , Taifa Stars  katika uwanja wa Taifa jijini DSM .

‘ hivi sasa tumeshakubaliana na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF  kuhusu mechi hii ya kirafiki ambayo inatarajia kuchezwa tarehe 22 mwezi Desemba “

Taarifa hii iemtolewa mjini Lusaka Zambia  katika Ofisi za ubalozi wa Tanzania wakati  akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Grace Mujuma.

Rais  wa  FAZ , amesema katika mechi hiyo ya kirafiki wa nampango pia wa kushirikisha kikosi kizima cha wachezaji wa timu ya wanachipolopolo   kwa lengo la kuifanya mechi hiyo iwe nzuri zaidi.

“Tuna mpango wa kushirikisha  kikosi kizma cha wachezaji  wanaocheza  ndani ya nchi ya Zambia na hali kadhalika wachezaji ia wanochezea  katika timu mbalimbali nje ya nchi , huu ndio mkakati wetu kabambe katika maandalizi ya michuano yanayokuja  nchini Afrika ya Kusini” alisema Kalusha

Aidha  amefafanua kuwa katika mechi hii ya kirafiki  kati ya Zambia na Tanzania wameona pia  waweke kambi maalum  ya amfunzo ya wiki nzima nchini Tanzania kwa lengo la kujiandaa  na michuano  inayotarajia  kufanyika  nchini Afrika ya Kusini mwakani .

Kwa upande wake Balozi  wa Tanzania  nchini Zambia Grace  Mujuma  amesema  kufanyika  kwa mechi hiyo ya kirafiki nchini Tanzania itakuwa  ndio nafasi ya kujipima zaidi kwa wachezaji wa Taifa Stars .

“Mchezo  huu utakuwa chachu kubwa kwa wachezaji wa Tanzania  kujipima na hali kadhalika kujifunza zaidi kwa wachezaji hawa  wa soka wa Zambia jinsi  gani wanavyocheza  mpira wa soka’ alisema Balozi Mujuma

Mujuma pia amewataka watanzania  mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuona mechi hiyo itakayokuwa  ya mfano wake  nchini Tanzania, kutokana na timu hiyo ya Zambia  hivi sasa imejipatia umaarufu mkubwa wa kushinda michuano ya AFCON 2012 .

Timu hiyo ya soka ya Zambia  imepanga kusafiri tarehe 16  kutoka mjini Lusaka Zambia na ndege ya Precision Airways  kuelekea jijini DSM  kushiriki mechi hiyo ya kirafiki  inayotarajia  kuchezwa  tarehe 22 mwezi DESEMBA  katika  uwanja wa kimataifa  wa mpira wa soka jijini DSM.
Posted by MROKI On Friday, November 23, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo