Akina
mama wa kijiji cah Nanguruwe mkaoni Mtwara ambao ni wanufaika wa mradi wa
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha wanawake
wanaonyonyesha na wajawazito fedha za kununulia chakula chenye lishe
wakijumuika na maofisa wa Vodacom kufurahia simu walizopatiwa zikiwa
zimeunganishwa na mtandao wa Vodacom kuwawezesha kupokea fedha za mradi kwa
njia ya M-pesa.
Afisa
Elimu Wilaya ya Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi akimkabidhi simu ya mkononi mmoja wa
wanufaika wa mradi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia
fedha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito fedha za kununulia chakula chenye
lishe kupitia M-pesa wakati wa uzinduzi uliofanyika juzi katika kijiji cah
Nanguruwe mkoani Mtwara.
Afisa
Elimu Wilaya ya Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi,akionesha aina ya simu iliyowekewa
fedha katika akaunti ya M-pesa zinazotolewa bila malipo kwa kwa akina mama
wanaonyonyesha kuwawezesha kupokea fedha za kunulnuia chakula chenye lishe
kupitia mradi wa Lishe bora na salama wa
shirika la mpango wa chakula duniani – WFP. Mradi huo umezinduliwa juzi katika
kijiji cha Nanguruwe, Mkoani Mtwara.
Baadhi ya wanufaika wa mradi wa
kuwawezesha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito mkoani Mtwara kupata chakula
chenye lishe akiijaribu simu aliyopatiwa ikiwa na fedha katika akaunti ya
M-pesa atakazozitumia kununulia chakula chenye lishe. Fedha na simu hizo
hutolewa bila malipo na Shirika la Mpango
wa Chakula Duniani – WFP kupitia mradi wake wa Lishe bora na salama.
0 comments:
Post a Comment