Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2012

Tembo katika hifadhi ya wanyama, Tarangire, kilomita 120 kutoka Arusha mjini, akionyesha mkonga na meno yake Jumamosi Oktoba 13, 2012.Wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, waliokuwa wakishiriki mkutano wa 22 wa Mfuko huo, walipata fursa ya kutembelea mbuga hiyo, baada ya ushiriki wa siku tatu mfululizo wa mkutano huo, uliotoka na maazimio  10 ya kufanya ili kuboresha huduma na ustawi wa mfuko
Mkurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kulia), akiongoza wanachama na wadau wa Mfuko huo kutembelea mbuga ya wanyama Tarangire, kilomita 120 kutoika Arushs mjini Jumamosi Oktoba 13, 2012. Wanachama na wadau hao walikuwa wakishiriki mkutano wa 22 wa Mfuko ambapo mkutano umetoka na maazimio 10 ya kufanya ili kuboresha huduma na ustawi wa mfuko
Wakurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Robert Mtendamema, (Aliyenyoosha mkono), ambaye anasimamia mifumo ya komputa ya Mfuko huo, Julius Mganga, nayesimamia utawala, (Kulia), na Steven Alfred, (Nyuma kulia), anayesimamia uwekezaji, wakitembelea mbuga hiyo Jumamosi Oktoba 13, 2012
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka Zambia, (Mwenye miwani), Mkurugenzi wa CITI bank, anayeshughulika na akaunti za mashirika, Gasper Njuu, (Watatu kushoto), na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakionyesha alama ya ushindi huku wakiwa kwenye gari la kitalii kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire mkoani Arusha Jumamosi Oktoba 12, 2012. Washiriki wa mkutano wa 22 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF walipata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii na mgeni huyo kutoka Zambia atyafikisha ujumbe nini amekiona kwenye mbuga hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dkt. Adiolf Mkenda, (Wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, (Kushoto), Mkurugenzi wa Utawala wa Mfuko huo, Julius Mganga, (Watatu kushoto), Mkurugenzi wa Mifumo ya Komputa ya Mfuko huo, Robert Mtendamema, (Wanne kushoto), na mjumbe wa bodi hiyo ya wadhamini, Frank Godfrey Mtosho, wakibadilishana hili na lile, kwenye mapumziko mafupi ya safari ya kilomita 120 kutoka mjini ASrusha kwenda mbuga ya wanyama Tarangire Jumamosi Oktoba 13, 2012. Wanachama na wadau wa mfuko huo waliokuwa wakishiriki mkutano wa 22 walipata fursa ya kutembelea mbuga hiyo baada ya kazi ya siku tatu kupeana taarifa na kuweka mikakati mipya juu yab maendeleo yab mfuko huo mjini humo
Mshiriki akisoma kipeperushi chenye maelezo ya kina ya Mbuga ya Wanyama Tarangire, kwenye eneo la maelezo kwa wanaofika kutembelea mbuga hiyo Jumamosi Oktoba 13, 2012
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Jannet Ezekiel, (Kulia), ambaye pia ni mratibu msaidizi wa mkutano wa 22 wa wanachama na wadau wa Mfuko huo uliomalizika Ijumaa mjini Arusha, akiwa na mwenzake, mapema Jumamosi nasubuhi, wakiandaa safari ya washiriki wa mkutano huo kwenda kutembelea mbuga ya wanyama Tarangire mjini Arusha
Wadau na wafanyakazi, wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa wamebeba chakula cha mchana :Lunch box" tayari kwa kula
Wafanyakazi na wadau wa Mfuko huo wakijipatia mlo kwen ye mgahawa wa Tembo ulio ndani ya hifadhi ya mbuga ya Tarangire
Wafanyakazi na wadau wa Mfuko huo wakijipatia mlo kwen ye mgahawa wa Tembo ulio ndani ya hifadhi ya mbuga ya Tarangire
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheniwa PPF, Adeligunda Michael Mgaya, (Kushoto), na Mwamini Tulli, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko mafupi ya safari ya kilomita 20 kuelekea mbuga ya wanyama Tarangire mkoani Arusha Jumamosi Oktoba 13, 2012
Wadau na wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakitembelea mbuga ya wanayama Tarangire Jumamosi Oktoba 13, 2012
Tembo na mkonga wake
Tembo mtoto akichookonoa shina la Mbuyu, huku Tembo mkubwa akiangalia wageni waliofika kuwashangaa kwenye mbuga hiyo. Mibuyu kwenye mbuga hiyo iko hatarini kuteketea kutokana na Tembo hao kuipekecha na kula mti huo ambao wataalamu wanasema huwa una majimaji na hasa wakati huu wa kiangazi amba;po maji ni hapa kwenye mbuga ya Tarangire

Swala Dume aliyetengwa na kundi lake akilalama
Punda Milia, akipita kwenye mto Tarangire huku ombo lake likiakisiwa kwenye maji ya mtu huo Jumamosi Oktoba 13, 2012. Watu walio karibu zaidi na wanyama wanasema, maajabu ya Punda Milia, ukiwatazama rangi zake  nyeupe na nyeusi huwezi kuwatofautisha, lakini tofauti yao inakuja jinsi michoro yake inavyopishana baina yao
Fundi Chuma au kwa lugha ya kitaalamu Hamerkop, mmoja anaonekana akifurahia juu ya mgongo wa mwenzake kwenye buga ya wanyama Tarangire Jumamosi Oktoba 13, 2012. Sifa na maajabu ya ndege huyo mwenye kichwa cha ajabu mithili ya nyundo ana uwezo wa kujenga kiota kikubwa zaidi kuliko ndege yeyote mwingine duniani
Bonde la mto Tarangire, ambao ndio tegemeo kubwa la wanayama kujipatia maji ya kunywa, lakini hadi camera yetu inatembelea mbuga hiyo Jumamosi Oktoba 13, 2012, mto huo umekauka, na kiasin kidogo cha maji kinaonekana
Ngedere alila ndizi mbivu, lakini ndizi hii hakupewa na mtu bali aliipora kutoka kwa watu waliokuwaakijipatia chakula cha mchana kwenye mgahawa wa Tembo Fast Food, ulioko kwenye lango la kuingilia mbuga ya wanyama ya Tarangira mkoani Arusha, Jumamosi Oktoba 13, 2012. Mbuga ya wanayama ya Tarangire yenye ukumbwa wa kilomita za mraba 2,850 na iko umbali wa kilomita 120 kusini mashariki mwa mji wa Arusha na iko umbali wa kilomita 160 kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro. Mbuga hiyo ni ya tano kwa ukubwa ukilinganisha na mbuga zingine hapa Tanzania. Kwa mujibu wa kipeperushi cha Mamlaka ya usimamizi wa hifadhi za taifa TANAPA, mbuga ya Tarangire ndiko kunakopatikana Tembo wengi zaidi
Mnyama atembeae kwa madaha, Twiga, akivinjari kwenye mbuga hiyo Jumamosi nOktoba 13, 2012. Kwa mujibu wa wafuatiliaji wa maswala ya wanayama pori, Twiga hulala shingo ikiwa wima. MORE PHOTOS: K-VIS BLOG
Posted by MROKI On Saturday, October 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo