Nafasi Ya Matangazo

October 26, 2012

WAREMBO 30 wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 usiku wa leo katika Hotel ya Girraffe Ocean View watachuana vikali kuwania taji la Miss Talent 2012 ambapo mshindi pia atapata tiketi ya kuingia moja kwa moja katika nusu fainali ya shindano la Miss Tanzania 2012.

Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo la tatu kufanyika ndani ya Miss Tanzania 2012, Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye amesema wanataraji mchuano mkali hasa kutokjana na warembo wengi kuwa na vipaji.

“Maandalizi yote yamekamilika na tunawakaribisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuja kushuhudia vipaji vya warembo mwaka huu na maandalizi yamekamilika,” alisema Makoye.
 
Ushindani mkali unataraji kuwepo kwa baadhi ya warembo ambao tayari wamekuwa wakionesha vipaji vyao mara kwa mara jambo ambalo linaleta changamoto kubwa kwa majaji wataakao ongoza shindano hilo.

Baadhi ya warembo ambao leo hii wanataraji kushindana vikali kuwania taji hilo ni Mrembo kutoka Kanda ya Ziwa, Babylove Kalala ambaye anautaalam wa hali ya juu ya kucheza ngoma za asili sambamba na kutumia nyoka katika uchezaji huo wa Ngoma.

Irine Veda kutoka Kanda ya Mashariki tangu mashindano ya Kanda amekuwa mataalam na mwenye kipaji kikubwa cha kupuliza Saxophone “Mdomo wa Bata” huku mrembo kutoka Kanda ya Ilala, Noela Michael na Zuwena Nasib kutoka Chuokuu Huria  wakiwa na kipaji cha uimbaji wa hali ya juu pamoja na  warembo mbalimbali ambao pia watashiriki shindano hilo kwa kucheza mziki na kuimba.

Taji la Miss Talent 2011 linashikiliwa na Mrembo Rose Albert kutoka Kanda ya Kaskazini.
 
Mshindi wa Shindano la Talent ataungana na warembo wengine watatu ambao tayari wameshapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya Redds Miss Tanzania 2012, ambao ni Lucy Stephan (Redd's Miss Photogenic),Mary Chizi (Redd's Miss Tanzania Sports Lady) pamoja na Magdalena Roy (Redd's Miss Tanzania Top Model).

Fainali za Redds Miss Tanazania 2012 zitafanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, Novemba 3 mwaka huu.
Posted by MROKI On Friday, October 26, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo